Ilipoishia “Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko,ย kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada yaย kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayoย Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwaย kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza ungaย pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadiย hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20ย kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutulizaย kiu yangu.ย
“Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlangoย ukifunguliwaย
“‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisiย ili kusiwe na maswali. Endeleaย
SEHEMU YA SITA
“Haya namalizia kupika kikiwa tayari nitakuja kukuita”ย alisema Mama Nesha kwa sauti ya mbali akiwa Jikoni namiย nilimjibuย
“Sawa Mama” Basi nilipitiliza hadi Chumbani kwangu huku ileย kiu ikizidi kuongezeka hadi nilisahau kufunga mlango, nguvuย zilianza kuniisha nikawa nafungua kete huku nikiwaย natetemeka, nilikuwa nimekaa chini, nilifanikiwa kufunguaย kisha nilianza kuvuta madawa kwa pupa sana, kwakuwa nilikuwaย nimeshazoea wala hayakunipa shida sana.ย
Nilivuta kwa nusu saa hadi niliona akili ikisizi kama vileย nilikuwa nataka kuingia usingizini, kumbe Mama Nesha alikujaย Chumbani kuniambia kuwa chakula kipo tayari, aliniona nikiwaย ninavuta madawa sababu mlango ulikuwa waziย
“Jojo” alisema Mama Nesha kwa mshituko Mkubwaย
“Unatumia madawa ya kulevya Jojo?” Aliuliza kwa mshitukoย akiwa amenisogelea, alinikata hamu zote nikamtazama kamaย mwizi aliyefumwa akiiba, sikutaka Mtu yeyote ajuwe kuwaย nilikuwa natumia madawa ya kulevyaย
“Kumbe ndiyo maana ulipoteza fahamu kwa siku mbili ni sababuย unatumia madawa ya kulevya, hii taarifa nampa Baba Neshaย kisha naenda polisi sitaki uje utuletee matatizo” Alisemaย Kisha alianza kuondoka kwa haraka pale chumbani, kiukweliย madawa yaliniondoa utu wangu kabisa, nilibadilika kutokana naย Maisha niliyoishi mwote nilimopita, nilifikiria kumuuwa Mamaย Nesha
Haraka nilimkimbilia Mama Nesha hata kabla hajafika chumbaniย kwake, nilimkaba shingo yake kwa nguvu sana sababu madawaย yalikuwa yakinipa nguvu, nilihakikisha namuuwa Mama Neshaย bila huruma huku madawa yakishinikiza kufanya hivyo.ย
“Jooo Joo, unanii…uwaa” Alisema Mama Nesha lakini sikujaliย hata mateso aliyokuwa akiyapata, sikutaka kuingia matatizoniย kabisa. Niliendelea kukaba shingo yake hadi hatua ya mwishoย ambapo alilegea kabisa na kufariki. Nilipomuuwa Mama Neshaย ndipo akili yangu ya kawaida iliporejea, niliwaza kukimbiaย msala huo.ย
Haraka nilirudi chumbani kwangu, nilichukua begi na vituย vyangu vyote kisha niliondoka, nilikimbilia stendi nilipandaย gari ya kurudi Dar. Nilikuwa nimechanganikiwa kabisa, uzuriย ni kuwa Baba Nesha alikuwa amesafiriย
“Dada futa pua yako kuna uchafu” Alisema Mkaka aliyekaa sitiย moja na Mimi, aliuwona ule unga eneo la pua yangu ilaย hakujuwa kama ulikuwa ni Unga wa madawa ya Kulevyaย
“Asante sana” Nilijibu kisha nilijifuta haraka sana, ilikuwaย ni mishale ya saa 9 Mchana, nilifika Dar saa 1 Usiku.ย Sikujuwa niingilie wapi usiku ule, pesa iliyobakia ilikuwaย chache sana. Usiku ule niliona ni bora nitafute Gesti nilaleย
Nilipata gesti maeneo ya Temeke Mwisho kule kwa nyuma,ย nililala hapo Usiku huo hata sikukumbuka kula. Asubuhiย niliona taarifa ya habari ikielezea juu ya Mauwajiย niliyoyafanya ila uzuri ni kuwa hakuna aliyekuwa na pichaย yangu ila tu jina la Jojo ndilo lililo tajwa, nilimuona piaย Baba Nesha akisema kwa uchungu na maumivu makali sana,ย alielezea jinsi alivyoniokota Shambani kwake na kunifanyiaย wema, yalikutwa madawa ya kulevya kwenye kile chumba ambachoย nilikuwa nikiishi. Roho iliniuma sana ila sikuwa na jinsiย sababu tayari nilishaamuwa kukimbiza Maisha yangu vinginevyoย ningekamatwa na polisi.ย
“Nimekuwaje Mimi Jojo?” Nilisema kwa maumivu makali sanaย ndani ya moyo wangu, sikutegemea kabisa kama ningefikia hatuaย ya kuwa Muuwaji. Nilifikiria sana niliona ni bora nitafuteย pesa nirudi nyumbani kwetu ila sikuwa na kazi. Nilibakiwa naย shilingi Elfu 10 tu ambayo ilikuwa ndiyo pesa pekeeย niliyonayo, niliiangalia huku nikitafakariย
Ghafla mlango uligongwa, nilishtuka sana, nilihisi ni polisiย maana kesi ya kuuwa ni kubwa mno, niliulizaย
“Nani?”
“Nahitaji kufanya Usafi” nilisikia sauti, nilijuwa tu atakuwaย ni Mtu wa Usafi wa ile Gest, niliangalia saa ya ukutaniย niliona ni saa 3 asubuhi, muda wa Mimi kuondoka pale Gestย uliwadia, nilienda kumfungulia kisha aliniulizaย
“Unalipia tena au unaondoka?”ย
“Naondoka, ila nitarudi, naomba nikuachie Begi languย tafadhali”ย
“Mh! Labda ukamuombe yule Mkaka wa mapokezi maana mimiย sihusiki kabisa na hayo, muombe atakukubalia tu ilimradi kuweย na usalama”ย
“Usalama upo Dada yangu” Basi, kwakuwa nilikuwaย nimeshajiandaa, nilikuwa nimevalia suruali nyeusi na rabaย nyeusi, juu shati jeupe nilielekea Mapokezi kumuomba Mkaka waย Mapokezi anihifadhie begi languย
“Habari Kaka yangu”ย
“Salama” alinijibu akionesha sio Mtu wa Stori nyingiย
“Samahani Kaka yangu naomba unihifadhie Begi langu kunaย mihangaiko nikaifanye nikirudi nitalichukua” Nilisema kwaย kujiamini kama vile mfanyabiashara aliyetokea mkoani kuja Darย kununua bidhaa, yule Mkaka kwa umakini sana kisha aliniulizaย
“Kuna usalama?” Nilijichekesha kidogo kisha nilimjibu “Ndiyo Kaka yangu”ย
“Fungua tuone kuna nini!” Alisema akiwa ananikodolea machoย kama Askari wa Barabaraniย
Nilijiamini sababu sikuwa na chochote cha kushangaza,ย nilifungua begi nikatoa nguo zoteย
“Ni nguo zangu tu Kaka yangu”ย
“Sawa liache ila hakikisha unalirejea leo leo” Alinisistizaย kwa ishara ya Kidole, nilimuaminisha kuwa nitalifuata japoย sikuwa na uhakika maana hata sehemu ya kwenda kuliweka lileย begi sikuwa nayo, nilirejesha nguo kwenye begi haraka sanaย kisha nilimpatia lile begiย
“Asante Kaka yangu jioni nitarudi Baada ya Mizunguko”
Basi niliondoka pale, hadi kituo cha magari ya kuelekeaย Mjini. Niliona Magari ya Kariakoo, Tabata, Ubungo, niliona niย bora nielekee Ubungo maana jina hilo halikuwa ngeni kwanguย kuliko Kariakoo na Tabata.ย
Nilikuwa mwingi wa kuwaza, nilitoa ile Elfu 10 kisha kondaktaย aliniambia hana Chenji atanipatia mbele, basi nikatuliaย zangu. Nakumbuka ndani ya gari waliweka redio ya Cloudsย kipindi cha Leo tena ikawa inasikika ile habari ya Mimiย kumuuwa Mama Nesha.ย
Nilishtuka sana nikahisi kama nimegundulika kuwa ndiyeย niliyeuwa maana niliona kama watu wananiangalia kumbe hataย haikuwa hivyo bali ni wenge langu tuย
“Konda nashuka” Nilisema huku nikiwa kwenye hekaheka zaย kupishana na watu kwa nguvu ili nishukeย
“We Dada si ushuke taratibu” Alisema Mdada mmoja, walaย sikujali nilisukuma Watu hadi nilipofika mlangoni, hataย sikukumbuka chenji yangu nilishuka kisha niliingia mtaani,ย niliona kabisa nilikuwa nimechanganikiwa kabisa. Kilaย niliyekutana naye niliona ni Polisi na anakuja kunikamata,ย nikawa kama Chizi jumlisha na madawa ya kulevya amabyoย nilikuwa nikiyatumia. Ilikuwa ni maeneo ya Buguruni Sheli,ย niliongoza njia ya kuelekea Vingunguti kupitia kwa Mnyamani.ย
Nilitembea kwa umbali mrefu sana bila hata kuhisi kuchokaย hadi nilipofika Machinjio ya Vingunguti, nilishuka na ileย barabara ya kuelekea Barakuda, nilipofika Kwenye Darajaย nilituliza wenge langu. Nilikuwa wa hovyo sana kuliko hataย ninavyoweza kuelezea hapaย
Nilitembea taratibu, njaa ilianza kunichapa huku ile hamu yaย kuhitaji madawa ya kulevya ikizidi kuniingia. Kilaย aliyenitazama aligundua haraka kuwa nilipoteza uwezo waย kujiamini, rangi na asili yangu ya uarabu ilifunikwa naย mawazo nikawa kama Muarabu aliyefirisika. Ilifika mahali hataย viatu niliviona vizito, nilivivua na kuvishika mkononi,ย nilitafuta sehemu nikakaaย
Mwili ulijaa arosto ya Madawa ya kulevya mno, nilijilazaย chini ya Mti nikiwa nimejikunyata. Niliwaza nikutane naย Shonaa anisaidie lakini sikujuwa alikuwa akiishi wapi, sikuwaย na simu wala nilikuwa simfahamu Mtu yeyote ndani ya Jiji laย Dar-es-salaam.ย
Nilikuja kushtuka giza lilikuwa limeingia, mwili ulikuwaย hauna nguvu kabisa. Kumbe pale nilipokuwa nimelala palikuwaย ni maskani ya wavuta bangi, moshi wa Bangi ulipopita kwenyeย pua zangu nilijikuta nikisisimka sana, nilimuomba jamaaย aliyekuwa anavuta akanipaย
Niliivuta haraka haraka kama vile Mtu mwenye njaa kaliย anapopata chakula katika mazingira asiyoyategemea.ย
Wahuni wote walinishangaa sana kisha ukimya ukawa umetawala,ย hata sikuchukua dakika moja nilikuwa nimeumaliza ule msokoto,ย basi liliibuka shangwe kutoka kwao wakinisifu kuwa Mimi niย jembe. Nilicheka pia maana nguvu ilikuwa imeshaniingiaย mwilini, wahuni walikuwa ndiyo wanangu.ย
Basi tulikaa pale wakiwa wanapiga stori zao, kulikuwa naย ubaridi fulani hivi ambao kila nilipovuta Bangi nilihisi jotoย la kutisha lenye raha ndani yake. Kadhaa waliondoka akabakiaย Jamaa mmoja tu ambaye alianza kuniuliza maswali ya hapa naย paleย
“Unaitwa Nani mrembo?” Aliuliza akiwa anacheka cheka, alikuwaย tejaย
“Jojo”ย
“Oh Jojo jijooo…Hahaha! Naitwa Domingo, mimi ndiyeย niliyepiga kampeni zote za CCM mwaka 1890 Nchini Japani”ย Alisema, zilikuwa ni stori za kuchekesha sana ambazo kwa mudaย huo niliona zilikuwa kweli kwasababu nilikuwa muathirika waย madawa hivyo akili yangu ilijaa uteja mnoย
“Ha!ha!ha! Wewe ni noma” nilisema nikiwa ninafurahiย
“Sema nini Jojoo…twenzetu mageto tukale raha au unasemaje?”ย Aliuliza Domingoย
“Poaa” Nilijibu hata sikufikiria Chochote, Tuliondoka tukiwaย tunapiga Stori za ajabu ajabu zilizotokana na bangiย
Gheto lenyewe lilikuwa ni kiota kilichojengwa kwa mifukoย kando ya Mto msimbazi.ย
“Hili ndiyo ghorofa langu Jojo, nimekuelewa sana ujuwe”ย Alisema Domingo, Bangi zilinifanya nione ni kweli ghorofa,ย basi tulilala na kufanya mapenzi hapo bila hata kujuwa afyaย ya Domingo, Maisha yangu Mimi Jojo yalizidi kuharibikaย
Asubuhi, Bangi ilikuwa imeondoka. Nilijishangaa mahaliย nilipokuwa nimelala, huyo Domingo nilimtazama mara mbili,ย alikuwa amejawa na chawa kwenye mwili wake, alikuwa naย ukurutu wa kutosha alafu nywele zake zilibadili rangi na kuwaย za dhahabu kutokana na uchafuย
“Nini hiki Jojo?” Nilijiuliza, nilitema Mate, japo nilikuwaย teja lakini sikufikia hatua ya kuwa Mchafu. Haraka nilitafutaย viatu nikaondoka zangu pale nikamuacha Domingo akiwa amelala.ย Watu walioniona nikiwa ninatoka Pale walinishangaa kutokanaย na uzuri nilionaoย
Basi nilirudi kule Buguruni kwa kufuata ile barabaraย niliyokuja nayo Barakuda. Nilipoteza muelekeo wa Maishaย kabisa, Jojo hali yangu ilikuwa mbaya sikula Tokea nilipokulaย kule Rufiji, niliona Vijana waliokuwa wakiomba omba kwenyeย magari yaliyo kwenye foleni, nilijiangalia nikaona ni boraย nami nikaombe msaada mana kuna Wakati nilikuwa najitambuaย kabisa na kujuwa kuwa sipaswi kuyaishi maisha ya Utejaย
Niliomba kwenye gari moja badala ya Jingine, wengineย walinikebehi, wengine hawakutaka kunisikiliza kabisa, gari yaย mwisho nilimkuta Msanii mkubwa sana wa kike hapa Tanzaniaย ambaye siwezi kumtaja jina lake, alikuwa ndani ya gari nzuriย sana akiwa naye anasubiria gari zianze kuondoka, niligongaย kioo chake, alipofungua ndipo nilipomuona kwa uzuri,ย alinifanya nitabasamu sababu sikuwahi kumuona ana kwa anaย
“Nikusaidie nini?” Aliuliza huyo Msanii maana nilikuwaย namkodolea macho tu hata kusema nilikuwa siweziย
“Naomba msaada Dada yangu sina pa kuishi, sina kazi, nahitajiย kurudi kwetu Tabora” Nilisema, aliniangalia kwa muda mrefuย bila kusema chochote kisha alimgeukia Mwanaume aliyekuwa nayeย kwenye gari nahisi alimuuliza kwa ishara kama anisaidie auย aniache, yule Mwanaume alinitazama juu chini kisha akamwambiaย
“Mchukue”ย
“Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifunguaย mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingiaย nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu yaย kuulizaย
“Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha nilionaย kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti yaย kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni,ย nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipikiย ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwaย nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimuย wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Nini Kitaendeea?ย Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?ย
Usikose SEHEMU YA SABA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย
ย ย


11 Comments
Awesome thanks
๐๐๐
Daah imenoga atar kiongoz
Daaaah
Unge onganisha ya saba tu maana umetuacha na alosto
Lahaulaa
Daah imenoga atar kiongoz
Nimeipenda pia nimefunzwa kitu
Jojo jijooo๐๐๐ ila mateja bana
Sijui kwanini nakua n arosto ya hii kama Jojo na dawa zake
sehemu ya saba please
Mzigo hatari unazidi kuelekea pazuri keep it up…..