Ilipoishia “Mama umemyoosha sana”ย
“Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kileย sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufungukaย kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo Msichanaย Mshikilie hadi mwisho.”ย
“Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno”ย
“Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena”ย
“Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatuย kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,ย akaingia Mwanaume mmoja.. Endeleaย
SEHEMU YA TISA
“Nimebwana, naomba kujisaidia” Akasema Matilda huku akianzaย kujikojolea, Mlinzi akamwambia Matildaย
“Nenda haraka” Akasema na kumsindikiza hadi chooni, chooย hicho kilikua cha ndani.ย
Alipoingia huko alikua tayari ameshasoma ni namna ganiย anaweza akaondoka hapo, akapanda juu ya sinki kisha akapitaย katika kitundu kidogo ambacho kilikua juu kilichotumika kamaย Dirisha la Choo, akadondokea chini, yule Mlinzi akaendeleaย kusubiria hapo huku mwenzake akiwa anamwita. Matilda akapataย maumivu kadhaa, jua lilikua linaanza kuzama, akatazama mbeleย yake akaona ukuta ambao haukua mrefu sana, akafikiria kutumiaย ukuta ili atimke hapo, akaparamia ukuta.ย
Mlinzi akaona dakika zinasogea akagonga mlango, akajibiwa naย ukimya huku akianza kupata mashaka juu ya uwepo wa Matilda,ย ikabidi afungue mlango, hakumkuta Matilda, akatazama paleย kwenye kitundu akaona dalili za Mtu kupitia hapo, akapandaย kwenye sinki akamwona Matilda akiwa anamalizia kuteremkaย ukuta, akagongana naye macho. Matilda akajiachia, Yule Mlinziย akatoka chooni akampa taarifa yule Mlinzi mwingine kishaย wakaelekea nje kwa ajili ya kuhakikisha wanamkamata Matildaย jioni hiyo.ย
Matilda akajikuta yupo Msituni, akaanza kukata nyikaย kuwakimbia walinzi hao ili asalimishe maisha yake, Walinziย wakiwa na mbwa wakawa wanamfukuzia Matilda ambaye alionekanaย kua na spidi kubwa sana, alikua kilomita kadhaa kutoka walipoย walinzi. Akaendelea kukata nyika huku giza likiwa linaingia,ย akawa amechoka sana, alikua hajui ni mahali gani alipo, hivyoย alikua akikimbia kama mwendawazimu tu.
“Mama nilitereza naomba unisamehe kwa hili, nilikosea kabisa,ย nipo tayari kulipa kwa hili, nakiri Mimi ni Mtoto mpumbavuย sana” Alisema James akiwa mbele ya Mama yake ambaye alikuaย amekunja uso wake, watu kadhaa walikua wameshafika hapo kwaย ajili ya Msiba wa Patra. Chozi na makamasi yalikua yakimtoka,ย Mama Naomi akamwonea huruma sana, akamtazama Mama Jamesย lakini hakua na nguvu ya kusema chochoteย
“Mamaaaaa!” akaita James huku akizidi kudondosha chozi, Mamaย yake alikua kimya sana akiwa anatazama pembeni, kwa hasiraย aliyokua nayo hakutaka kabisa kumtazama Jamesย
“Mama James, rudisha moyo wako nyuma, huyu ni Mtoto,ย ameteleza” Akasema Mchungaji George ambaye alikua bega kwaย bega na familiaย
“Tunazungumzia Maisha ambayo hayawezi kurudi, yule Binti,ย hawezi kurudi kwa namna yoyote ile, na Mama yake piaย asirudi?” akauliza Mama yake James huku akiwa amekaza machoย yake kwa Mchungaji George, Mchungaji akameza funda la mate,ย swali aliloulizwa lilimfanya akae kimya.ย
Chozi na jasho vilikua vikivuja kwa pamoja, James alijitahidiย sana kumwomba Mama yake amsamehe lakini Mama Jamesย akashikilia msimamo kua hawezi kumsamehe hadi Matildaย aonekane. James akaondoka hapo Usiku
Hekaheka ndani ya Msitu ilikua ikiendelea, Matilda aliendeleaย kuwakimbia wale walinzi wa Neema, alichoka akaamua kujibanzaย nyuma ya Jiwe kubwa, walinzi nao walikua wameshachoka hukuย wakihimizana kua kabla ya jua kuchomoza wahakikishe kuaย wamempata Matilda.ย
Matilda akalala hapo Msituni hadi siku iliyofuata, alipoamkaย akaendelea na safari ya kutafuta msaada wa kutoka hapoย Msituni, akakatiza vijito na majabari makubwa na madogo hukuย akiwa hajui ni wapi anaelekea.ย
Moyoni mwake akawa anasema na Mungu wake kua amlinde Bintiย yake, Masikini hakujua kua Binti yake alikua ameshafariki,ย ghafla akasikia sauti za Mbwa akajua anapaswa kuongeza mwendoย wa kuendelea kuutafuta Msaada, akakimbia umbali mrefu akiwaย na njaa na kiu ya Maji akajikuta akianguka baada ya kuhisiย kizunguzungu.ย
“Eee Mungu nilinde” Akasema Matilda, akahisi giza kishaย akapoteza fahamu.ย
“Babu kinachofuata ni kitu gani?” Akauliza Neema, Babu naย Mama yake wakiwa mbele yakeย
“Mtoto akizikwa habari yake itakua imeisha pia, James anaendaย kua mali yako bila kipingamizi chochote kile, hili ndiyoย jambo kubwa” Akasema Babu yake Neema, wakafurahi sanaย
“Yaani Babu kama tutafanikisha hili nakuahidi kua nitakupaย zawadi ambayo hutonisahau” Akasema Neemaย
“Huna haja ya kuahidi sababu wewe ni Mjukuu wangu Neema,ย kikubwa upate unachohitaji, ukipata wewe Mama yako amepata,ย basi ndiyo furaha yangu hiyo”ย
“Pamoja na hayo Babu nitahakikisha nakujengea nyumba yaย kifahari, nitakua na pesa nyingi” Alisema Neema. Mama Neemaย alikua Mtu wa kutabasamu tu akimwangalia Mwanaye na Babu yakeย wakiwa wanazungumza, kicheko chao kilikua kilio upande waย Mama James ambaye kila alipofikiria jinsi mambo yalivyoendaย alijikuta akiangusha kilio cha Mtu mzima.ย
Moyoni alijua kua kuendelea kuzuia Mtoto kuzikwa ni sawa naย kumtesa Mtoto huyo lakini moyoni pia alikua akiumia Mtotoย kuzikwa bila Mama yake kuwepo, aliona ni sawa na kuzuia hakiย ya Msingi ya Mama Patra, lakini hakuna aliyejua kilichokuaย kikiendelea, Matilda alikua akipigana vita Msituni.
“Nipo wapi?” Akauliza Matilda baada ya kujikuta akiwa kwenyeย nyumba moja ambayo ilikua imeezekwa makuti, hakuna aliyeย mbele yake bali kitanda na ukuta uliojengwa kwa udongo waย kugandika. Akakohoa kidogo, haraka akaingia Mzee Mmoja ambayeย alikua na ndevu ndefu, chafu zenye Mg’ao wa fedha, alikua naย rasta pia, Matilda akaogopa sana, wakati anajisogeza pembeniย akajikuta shuka ikiwa inamvuka, ndipo akagundua kua alikuaย hana nguo yoyote ile, akarudisha macho kwa mzee kwa Mshangaoย
Mara, akaingia Bibi mmoja ambaye alionekana wazi kua ni Mkeย wa Mzee huyo.ย
“Usiogope Binti, Nilikukuta ukiwa hujitambui nikakusaidia”ย Akasema Mzee huyo, Bibi akaketi pembeniย
“Na wale watu waliokua wakinifukuzia?” Kwanza Bibi akacheka “Walishambuliwa na jeshi langu” Akasema Mzee huyo “Jeshi lako, unamaanisha nini?”ย
“Siafu waliwashambulia walipotaka kukuchukua, wakakimbiaย ndipo nikakusaidia” Hadithi hiyo ikamshtua sana Matilda.ย
“Umepoteza fahamu kwa zaidi ya masaa matano, unahitajikaย kupumzika zaidi ili kuvuta nguvu, lakini kwanini wale Watuย walikua wakikufukuzia?” Akauliza Bibiย
“Ni stori ndefu sana” Akasema Matilda baada ya kuona watu haoย si wabaya kwake, akawasimulia kilichotokeaย
“Pole lakini unaonekana bado una tumaini kwa hayo unayopitia,ย bado una Muda wa kurekebisha mengi” Akasema Babu huyo,ย Matilda akaketi vizuriย
“Unamaanisha nini Babu”ย
“Ulipokua umelala nilifanikiwa kuyaona yanayokuzunguka,ย usishtuke sababu ipo Dunia isiyoonekana, ni Dunia ambayoย mambo huenda haraka mno, huyo Mtoto unayemzungumzia hapa yupoย kwenye usingizi mzito sana, hawezi kuamka kirahisi sababuย nguvu kubwa imetumika kumlaza” Akasema Babu huyo, Matildaย akashtuka sana
“Usingizi?, kwanza niko wapi hapa nataka kwenda kumwona Bintiย yangu”ย
“Hapa ni Mkata”ย
“Mkata?”ย
“Ndiyo, kilomita kadhaa kutoka hapa kuna barabara ambayoย inaelekea huko ulikotoka”ย
“Umesema kuhusu Usingizi, sijakuelewa”ย
“Namaanisha Mtoto wako amekufa katika Dunia hii lakiniย anaishi kuzimu” Matilda akazidi kushtuka, aliyokua akiambiwaย yalimpa Mshtuko mkubwa sana, chozi likaanza kumtokaย
“Mtoto wangu amekufa?”ย
“Ndiyo lakini usilie sababu bado hajaondoka, mwili umekufaย lakini nafsi inaishi kuzimu, kikubwa unatakiwa kuwahi kablaย hajazikwa”ย
Wazee hao wakamwambia mengi sana Matilda, wakampa chupa yaย Maji, wakamwambia kua akifika anyunyize maji kwenye mwili waย Binti yake, ataamka na kua sawa kabisa.ย
Haikuishia hapo, wakampa nauli ya kurejea Dar.
“Mchungaji, naona namtesa Mjukuu wangu, hakuwa na kosa loloteย sitaki aendelee kuteseka zaidi. Kesho Patra azikwe” Akasemaย Mama yake James, alizungumza mbele ya Jamesย
“Asante Mama, najiona nimepoteza thamani kubwa sana katikaย Maisha yangu. Nitamtafuta Matilda kadiri ya uwezo wangu Mama”ย Akasema James, Siku iliyofuataย
Taratibu za Mazishi zikafanyika, mwili wa Patra ukawekwaย kwenda sanduku, vilio vilitawala, familia ilizizima, Jamesย alilia sana mbele ya sanduku la Patra, alijutia sanaย kumkataa, akatamani hata aamke ili amuombe msamaha Bintiย yake, kila aliyefika aliona ni jinsi gani James alikua katikaย hali mbaya sanaย
Mchungaji George akaongoza maombi ya ibada ya mazishi yaย Patra, hatimaye sanduka la Patra likawa linashuka taratibuย kuelekea chini, ikasikika sauti ikisema
“Patraaaaaaaa” Ilikua ni sauti iliyotambulika kwenye masikioย ya walio wengi, vilio vilikoma, hakuna aliyeamini, walimwonaย Matilda akiwa ameshikilia chupa aliyopewa kule Msituniย
“Msimzike Binti yangu bila kumwona” Alisema Matilda,ย Mchungaji akawaamuru waliokua wakishusha sanduku kulirudishaย juu, Matilda akakimbia hadi kwenye sanduku la Patra, kishaย akageuka na kuwaambiaย
“Patra hajafa msimzike” Alisema akiwa anatokwa na mchoziย
Ni kama watu walipigwa Bumbuwazi, hakuna aliyesema chochoteย zaidi ya Mchungaji George ambaye alimuuliza Matildaย
“Unasema nini Matilda, Mtoto amekaa kwenye jokofu kwa sikuย tatu. Ulikua wapi?” Akaulizaย
“Mchungaji, moyo wangu unaniambia nimwone kwanza Mtoto ndipoย nieleze kilichotokea, chozi la James lilijikuta likikaukaย lenyewe kutokana na Mshangao ambao alikua nao, minong’onoย ikaanza kusambaa miongoni mwa waliofika Kwenye mazishi.ย
Mchungaji akawaambia walifungue sanduku ili Matilda amwoneย Mtoto wake, sanduku likafunguliwa, Matilda akafungua chupa yaย Maji akanyunyiza kwenye sandukuย
“Unafanya nini?” Akauliza Mchungaji Georgeย
“Patra ataamka sasa hivi” Alisema Matilda, Mchungaji akaonaย Matilda amechanganikiwa, akawaamuru wannaume kumshika Matildaย ili Sanduku lifungweย
“Mchungaji mwanangu ni mzima naomba Msimzike” alisemaย Matilda, ukimya ukatawala kwenye sanduku, alichotegemeaย Matilda kilikua ni sawa na njozi ya mchana, Patra hakuamkaย kama alivyofikiria, akaanza kuona wale wazee walikuaย wamemuongopea, alilia sana huku utaratibu wa kulifungaย Sanduku ukifanyika, Mama Naomi akamwambia Matildaย
“Mtoto amekufa Matilda hawezi kurudi” Mchungaji akamsogeleaย Matilda akamwambiaย
“Huu ni mwisho wa Patra lakini siyo mwisho wa Maisha yako,ย pole kwa msiba”ย
Katika hali ambayo kila mmoja alistaajabu, Patra akaamkaย kwenye sanduku na kukaa kitako kitu ambacho si tuย kilimfurahisha Matilda bali kilimshtua, tokea amezaliwaย hakuwahi hata kukaa lakini aliamka na kuketi kiisha akaanzaย kushangaa watu. Wasio na moyo wa ujasiri walikimbizanaย Makuburini, wachache wakabakia.ย
Muda huo Babu yake Neema alikua amepata ishara mbayaย akamwambia Neemaย
“Nenda Muhimbili kaokote kile kitu kakitupe jalalani harakaย sana”ย
“Babu kwanini unasema hivyo?” Akauliza Neemaย
“Nenda Neema fanya haraka sana” Akasistiza Babu yake Neema,ย haraka Neema akakodi Pikipiki ili awahi Muhimbili,ย haikuchukua muda mrefu, akawa amefika Muhimbili, akakimbiliaย mahali ambapo alitupa kile kitu, kabla hata hajakiokotaย kikawaka na kumwingia machoni, akawa anapiga keleleย akilalamika kua haoni, haraka akasadiwa kupelekwa Kwaย Daktari.ย
Familia ikawa imekaa, kila mmoja akistaajabu maajabu ya Mtuย aliyekufa kurejea tena kwenye Maisha, ukimya ukawa mwingiย sana. Matilda akaanza kuwasimulia kila kitu, siku hiyo ndiyoย ikawa siku ya kumwona Mama yake James, huwezi amini Patraย alikua ni Mtoto mrembo sana, akitabasamu ni James Mtupu,ย James akaomba Msamaha na kuahidi kua atafunga ndoa na Matildaย na kumlea Mtoto.ย
Zikapita siku tatu mambo yakawa shwari, furaha na amaniย ikazidi kutamaraki, kwa shukurani, James akampatia Mama Naomiย ile nyumba aliyokua akiishi Matilda, akampa pesa pia kwaย ajili ya kuanza Biashara. Siku moja akiwa ofisini akapokeaย simu ya Mama Neema, alivyopokea akaambiwa kua Neema amepofukaย macho, James akamwambia kua ataenda kumwona.ย
Baada ya kazi akaenda Hospitalini kumwona Neema, Mama Neemaย akiwa analia sana kwa kile kilichomfika Binti yake.ย
“Mama huna haja ya kulia, Mimi nimelia sana, Matilda ameliaย sana, Mama yangu amelia sana. Siku zote Mshahara wa dhambi niย umauti Mama”ย
“Lakini James, Neema ana Mtoto wako tumboni, hupaswiย kumhukumu moja kwa moja”
“Namshukuru Mungu sababu amefumbua fumbo zito sana, sikuwahiย kuwa na thamani kwenu hata kwa yale makubwa niliyowafanyia,ย nilikua mjinga sijui hata nilikwama wapi hadi nikamkataaย Mtoto wangu wa damu” Akasema James kisha akataka kuondokaย
“James, naomba msaada kama Mama, Neema anatakiwa kwendaย kutibiwa India, sina pesa hiyo Mwanangu, msaidie kwa hilo tu”ย
“Siwezi kumsadia adui anayewinda Maisha yangu, alie mbele yaย Mungu wake, amwombe amsamehe” Akasema James kisha akaondoka,ย Mama Neema akalia sana huku akijilaumu kwa kusema ni ujingaย wake kwani yeye ndiye aliyekua akimshauri vibaya Binti yake,ย akaona ni bora kufa kuliko kuendelea kumwona Neema akiwaย kipofu, akaondoka Hospitalini na kumwacha Neema akitesekaย kwenye kutanda cha Hospitalini ya Muhimbili.ย
MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
ย
18 Comments
Adminiiiiiiiii hongera sanaaa ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ๐ฅณ dah mwisho mzuri ..kesho anza riwaya nyingine
Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi
Kali sana
Safi sana mwisho nzur riwaya ilikuwa ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Daah riwaya nzuri Sana
dah story moja nzuri sana
Asante Mungu wamepata wanachostahili๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Mmmmmmm,, mbona imeisha kama inaendelea????????!!?????
Big up Admin!
Riwaya unazotupatia zinatupa fundisho katika maisha halisi yanayotuzunguka.
Hongera sana mkuu kwa story nzuri sana
Dah hatari sanaaaaa
Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi
๐ฅ๐ฅ sio powa imeisha kama utani
Hongera san kiongozi ๐๐๐
Tujitahid kumtunza admin asivunjike moyo wakutupa madini mazuri kma hya
๐๐โค๏ธ
Admini safi kesho anza nyengine
Imeisha vibaya wazaz wake ma patra je