Ilipoishia “Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwaΒ kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua niΒ James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee HospitaliΒ kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. AkaketiΒ kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namnaΒ mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari yaΒ Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini JamesΒ alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepakiΒ sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingiaΒ akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. EndeleaΒ Β
SEHEMU YA NANE
Hofu ikatanda kwenye moyo wake sababu Neema alishasema kuaΒ atamuuwa Patra, katika hali isiyo ya kawaida James akajikutaΒ akiumia ndani ya moyo wake, akatamani kushuka ili amfwatilieΒ lakini moyo wake ukawa unamsuta mara kadhaa huku akimshuhudiaΒ Neema akishuka na kuanza kutembea kwa Mguu kuelekea ndaniΒ zaidi. Akawa kwenye vita kubwa sana ndani yake hadiΒ aliposhinda na kuamua kushuka kisha akaanza kumfwatiliaΒ Neema, kumbuka Neema alikua amepewa ile dawa na Babu yakeΒ akaiweke katikati ya Hospitali ya Muhimbili ili Mtoto PatraΒ aonekane kusudi auaweΒ
“Huyu amefwata nini hapa Hospitalini?” akajiuliza James akiwaΒ anaendelea kumfwatilia, James alifahamu mahali alipolazwaΒ Patra, Neema akawa anaelekea huko pasipo kujua kua ndikoΒ aliko Patra, lakini baadaye akabadilisha uelekeo kitu ambachoΒ kilimfanya James ashushe presha yake. Neema alikua makiniΒ sana tena akionekana ni mwenye kujiamini kabisa, JamesΒ hakutaka kukubali kushindwa akataka kujua ni jambo ganiΒ limempeleka Neema Hapo Hospitalini.Β
Matilda akiwa katika chumba chenye giza, hakujua mahali hapoΒ ni wapi isipokua alijua kua alikua amehamishwa kutoka paleΒ alipokua zamani, alimfikiria sana Binti yake, akawa anasikiaΒ walinzi wakizungumza, tena wakibishana masuala ya Mpira,Β Chumba alichopo hakikumpa ruksa ya kuona kilichokuaΒ kikiendelea nje isipokua aliisikia kelele za hao walinziΒ pekee, alijua yupo mafichoni, akaanza kupiganisha akili iliΒ ajue anaweza vipi kutoroka hapo.Β
Basi, James akaendelea kumfwatilia Neema taratibu tena kwaΒ umakini huku akiwa na maswali mengi sana kichwani. Neema nayeΒ akazidi kuongeza mwendo huku lengo likiwa kufanya kamaΒ ambavyo Babu yake alimwambia, alipofika katikati yaΒ Hospitali, akageuka huku na kule huku James akijibanza mahaliΒ ili aone Neema anaelekea wapi.Β
Akazuga kidogo kabla ya kuingiza mkono kwenye Mkoba kishaΒ akatoa hicho alichopewa na Babu yake alafu akakitupa naΒ kukificha kwa Majani kwa kutumia Mguu wake, James alikuaΒ akiona kila kitu, baada ya kumaliza akaangaza tena huku naΒ kule kisha haraka akageuka na kurudi alipotoka, akampitaΒ James bila kumwona kisha akaelekea Kwenye maegesho lakiniΒ wakati anatoka hapo akaliona gari la James ndipo akapataΒ uhakika zaidi kua Patra yupo hapo Hospitalini, akatabasamuΒ kisha akampigia simu Babu yake na kumwambia kua ameshamaliza,Β kweli Babu yake alipoangalia tena alimwona Patra kishaΒ akacheka na kutengeneza bomu kwa ajili ya kummaliza PatraΒ
James akafikiria sana ni kitu gani ambacho Neema alikiwekaΒ pale, hakutaka kukipa uzito sana badala yake akarudi nyumaΒ kisha akaelekea ilipo wodi ambayo Patra amelazwa, kumbukaΒ ndani ya wodi hiyo alikuwepo Mama yake MzaziΒ
Basi James akasogea hadi mlangoni, Patra alilazwa katika wodiΒ ambayo ilikua ya hadhi kubwa sana, kitendo cha kufika tuΒ mlangoni alifanikiwa kumwona Mama yake Mzazi akiwaΒ anazungumza na Mchungaji, alimwona kupitia kioo cha hapoΒ Mlangoni, akashtuka sana, Mara akashikwa begaΒ
Akageuka na kukutana na Daktari ambaye alikua amezungumzaΒ naye na kumwambia kua kwa lolote litakalo hitajika basiΒ amweleze, na ndiye aliyekua akimweleza kuhusu hali ya MtotoΒ
“Oooh Mr. James….Karibu sana” Alisema Daktari kisha akampaΒ mkono James ambaye alikua katika butwaa zito sanaΒ
“Ndiyo unakuja au unaondoka?” akauliza Daktari huyo, BadoΒ James alikua kwenye Butwaa maana hakutegemea kumwona MamaΒ yake pale Wodini.Β
“Nili….kua…Naondoka” Akasema James kwa kujiuma umaΒ
“Basi sawa, namshukuru Sana Mungu hali ndiyo kamaΒ ulivyoiyona, Mtoto anaendelea vizuri kwasasa” Akasema DakatriΒ kisha akafungua mlango na kuingia wodini, Haraka JamesΒ akaondokaΒ
“Mmemwona Mfadhili?” akauliza Daktari, wote wakashangaa “Mfadhili?” akauliza Mama yake JamesΒ
“Ndiyo…..si alikua hapa kumwona Mtoto, ametoka sasa hiviΒ nimepishana naye hapa Mlangoni”Β
“Hapana Dokta, Hakuna Mtu aliyefika hapa wodini tokeaΒ ulipotuacha” Akasema Mama yake James, ikampa Mshangao Dokta,Β akaelekea mlangoni kumwangalia James lakini hakufanikiwaΒ kumwona tena
“Mbona nimekutana naye mlangoni akanambia kua ametoka hapaΒ wodini, yeye amekua akichangia pesa za matibabu ya Mtoto”Β Alisema, kisha akatoa Kadi ya Biashara ambayo alipewa naΒ James, akamwonesha Mama James, ndipo Mama James nayeΒ alipogundua kua James alikuja Hospitalini na bila shakaΒ alimwona Mama yake, lakini kilichomshtua Mama James niΒ kusikia kua James anachangia matibabu ya Mtoto.Β
Muda huo tayari James alishaondoka Hospitalini, alikuaΒ Barabarani akiendesha gari yake kwa sapidi sana kuelekea njeΒ ya Jiji ambako alimwacha Matilda, hakujua kua MatildaΒ alishaondolewa. Alitumia masaa zaidi ya mawili hadi kufika,Β alipoingia ndani ya jumba hilo lililo msituni hakumwonaΒ Matilda pia hakukuta Mtu yeyote yule kitu ambacho kilianzaΒ kumchanganya. Akaingia tena kwenye gari na kurudi MjiniΒ
Wakati huo Matilda akiwa bado anapiganisha akili anawezajeΒ akatoroka hapo ili kunusuru Maisha yake, Walinzi walikuaΒ wakikagua chumba chake mara kwa mara kuhakikisha haondokiΒ hapo kama ambavyo Neema alikua ameagiza, ilimpa wakati mgumuΒ sana MatildaΒ
Mama yake James aliporudi nyumbani kwake alihisi mwiliΒ ukipata moto, kwanza kujua tu kua James amshamwona paleΒ Hospitalini kulimpa mashaka makubwa sana sababu hakutakaΒ ajuwe chochote lakini kingine kilichomuwazisha zaidi ni paleΒ aliposikia kua James alikua akitoa pesa za matibabu ya Mtoto,Β maana yake ni kwamba James alikua na mapenzi na Patra.Β
Siku iliyofuata mapema sana, taarifa mbaya ilianza kueneaΒ kwenye simu, ilikua ni kuhusu hali ya Patra ambayoΒ ilibadilika ghafla sana, tena ikidaiwa kua mapigo yake yaΒ moyo yalikua yakishuka kwa kasi kitu ambacho kilikuaΒ kinaashiria kifo kwa Mtoto huyo, miongoni mwa waliotumiwaΒ ujunbe huo alikua ni James, Mama yake James, Mama Naomi, JackΒ na Mchungaji GeorgeΒ
Haraka wote wakafika Hospitalini isipokua James ambaye alikuaΒ akifikiria ni namna gani ataingia hapo kwa ajili ya kumwonaΒ Patra, ilionekana wazi kua Patra anaweza kutangazwa kuaΒ amefariki muda wowote, Mchungaji alijitahidi sana kufanyaΒ maombi lakini Mishale ya saa nne Asubuhi Patra alifarikiΒ Dunia, Daktari akathibitisha hilo
“Poleni sana, tumejitahidi kuokoa uhai wake lakini juhudiΒ zetu zimegonga mwamba” Akasema Daktari huku akishuhudia mvuaΒ ya vilio, Mchungaji George akashindwa kuvumilia akakimbiliaΒ kulia nje kama Mwanaume, ilikua ni huzuni kwa kilaΒ aliyesikia. Mama James hakuona kama kulikua na sababu yaΒ kuendelea kulificha hilo sababu alihitaji msiba ukafanyikeΒ nyumbani kwake, akampigia simu James na kumwambia kuaΒ anahitaji kuonana nayeΒ
Haraka James akaenda nyumbani kwa Mama yake, akamkuta MamaΒ yake akiwa mwingi wa huzuni, akaketi kando ya Mama yake kablaΒ ya kumuuliza kiunyonge kilichopelekea huzuni hiyoΒ
“Amekufa” Alisema Mama yake James huku chozi likizidiΒ kumvuja, James akashtuka sana, moja kwa moja akajua ni PatraΒ lakini akajikaza huku akizidi kumuuliza Mama yakeΒ
“Nani huyo Mama”Β
“Mtoto wako, Kwanini ulifanya siri James, Mtoto ameteseka MnoΒ hadi amefariki” Akasema Mama yake James huku akiangushaΒ kilio, chozi likambubujika James, hakua na la kufanya,Β hakuweza kubeba ukatili wa kukana mbele ya Mama yakeΒ
“Kisa ulemavu James umegeuka kua Mnyama, Mama wa Mtoto hadiΒ sasa hajulikani yupo wapi….James, hapana shaka upo nyuma yaΒ hili jambo, nakuhakikishia kua Patra hatozikwa kama Mama yakeΒ Patra hatopatikana” Alisema Mama yake James, kila jamboΒ lilikua tayari limefunguka, hapakua na siri tena. JamesΒ akainamia chiniΒ
“Kama kuna siku nimeumia katika Maisha yangu James basi niΒ leo, James wewe ni katili sana Mwanangu, hustahili kuitwaΒ Binadamu, Nenda kamlete Mama yake Patra hapa” Akasema kwaΒ hasira Mama yake James, Basi James akawa kama Budi akasimamaΒ asijuwe aingilie wapi kumtafuta Matilda, akatoka huku choziΒ likiendelea kumbubujika, alipofika getini alipishana na gariΒ iliyowabeba Mchungaji, Mama Naomi na JackΒ
Alipotoka hapo James akaelekea Baa, akaagiza pombe kali naΒ kuinywa kama anakunywa maji, alihisi kufanya hivyo kungeondoaΒ Mawazo yote, licha ya kua na pesa nyingi ambazo wengi huaminiΒ kua na pesa kunamaliza matatizo lakini upande wa James ilikuaΒ tofauti, pesa ndiyo iliyoleta matatizo kwake.Β
Giza liliingia huku James akiendelea kuagiza moja baridi,Β moja moto hadi akalewa kabisa na kushindwa kujitambua,Β akasaidiwa na baadhi ya waliomjua sababu alikua maarufu,Β akarudishwa nyumbani kwake.
Usiku huo tafrani ikawa nzito nyumbani kwa Mama James,Β Mchungaji aliomba Patra azikwe lakini Mama James aligomeaΒ kabisa akihitaji kwanza Matilda afike ili amshuhudie BintiΒ yake, wakambembeleza sana lakini akagoma huku akiwaambiaΒ James atamleta Matilda sababu anajua ni wapi alipo na kamaΒ hatomleta basi Patra hatozikwa. Mama Naomi na MchungajiΒ wakatoka kwa ajili ya kuzungumzaΒ
“Huyu Mama anamaumivu makali sana, amemjua Mjukuu wake tu naΒ Mjukuu amefariki, hali aliyonayo ni ngumu sana kuelewaΒ chochote kile, cha Msingi kukipambazuka tumtafute JamesΒ pengine anajua ni wapi alipo Matilda” Akasema Mchungaji,Β Asbuhi mapema sana wakampigia simu James, wakapanga waonaneΒ ili kuweka mambo sawa, James hakua na ujanja akawaelekezaΒ mahali anapoishi, walipofika walikuta mazingira ya hovyo sanaΒ sbaabu wafanyakazi wote waliondolewa na Neema, aliyebakiaΒ alikua ni mlinzi tu ambaye alikua hafanyi usafiΒ
“Kilichotuleta hapa ni kuhusu Matilda, Mama yako amekataaΒ kumzika Mjukuu hadi pale Mama yake Patra atakapofika, JamesΒ kama unapajua alipo Matilda tafadhali tuambie ili tumsitiliΒ yule Mtoto” Alsema Mchungaji, Mama Naomi akawa anafuta choziΒ lakeΒ
“Mchungaji kiukweli sijui mahali alipo Matilda,, NimehangaikaΒ sana kumtafuta bila mafanikio yoyote yale, ilipofikiaΒ nimekata tamaa” Akasema James, hakutaka kabisa kusema kuaΒ Neema ndiye anayejua mahali alipo Matilda, sababu alihofiaΒ usalama wa Neema kwakua alikua MjamzitoΒ
“Mbona Macho yako yanasema ukweli lakini mdomo wako unaongopaΒ James, wewe ndiye ulimshtaki Matilda, akaenda polisi lakiniΒ akatoweka katika Mazingira tata, unajua alipo..” akadakiaΒ Mama yake Naomi kwa hasira sanaΒ
“Jamani ningekua najua alipo ningemleta lakini sijui alipo,Β nawaahidi nitaendelea kumtafuta” Akasema James huku akikunaΒ nywele zakeΒ
Mchungaji akasimama na kusemaΒ
“Kumbuka kua Mtoto hatozikwa kama Matilda hatopatikana”Β Alisema kisha akaongoza nje, Mama Naomi akamwambia JamesΒ
“Hadi kifo kinamchukua Mtoto ukiwa unaendelea kumkana, hakikaΒ wewe ni miongoni mwa matajiri wajinga sana Duniani” AlisemaΒ kisha naye akaondoka hapo, James hakua na jeuri tena sababuΒ alikua katika nyakati ngumu sana
Walipoondoka Mchungaji na Mama Naomi, James akaingia kwenyeΒ gari yake, akampigia Jack kua asimamie majukumu ofisini kishaΒ akawasha injini ya gari na kutimka hapo, kichwa chake kilijaaΒ mkanganyiko, zilipita siku mbili bila kuzungumza na Neema,Β akili yake ikawa inawaza atafanya nini ikiwa Neema ndiyeΒ anayemshikilia Matilda.Β
Injini ya gari ikazima katika geti la Nyumba ya Neema, MlinziΒ akatoka na kumwambia James kua hapaswi kuingia ndaniΒ
“Hivi unajua unamzuia Nani, Mimi ndiye niliyeinunua hiiΒ nyumba, hebu pisha” Akasema James kwa hasira, alihitajiΒ kuzungumza na NeemaΒ
“Hii siyo amri yangu, nimeambiwa nikuzuie James” AkasemaΒ MlinziΒ
“Bali ni amri ya Nani?” akahoji James, Mlinzi akachunguliaΒ ndani kisha akamwambiaΒ
“Neema”Β
“Neema? hebu nipishe..” Akasema James huku akijikutaΒ akisukumana na Mlinzi pale getini mara gari ya Neema ikafika,Β Neema alikua ndani ya gari hiyo, hakutaka kushuka, JamesΒ akasogea kisha akamwambia NeenaΒ
“Shuka nahitaji kuzungumza nawe” Licha ya James kusema kwaΒ jazba lakini Neema hakutaka kutii amri hiyo, alishajua niniΒ kimemleta James nyumbani kwake, James akafungua mlango naΒ kumchomoa NeemaΒ
“Wewe vipi kwani kuna ulazima wa kuzungumza na Mimi?” akahojiΒ kwa dharau Neema, James akampiga kibao Neema, ilikua ndiyoΒ mara ya kwanza James anampiga Neema, wakati huo Mama yakeΒ Neema alikua ameshatoka ndani, akamsukuma JamesΒ
“Wewe una Kichaa? unampiga ulimzaa wewe huyu?” akauliza MamaΒ yake Neema huku akimtaka James ajibuΒ
“Mama, Neema ananiletea dharau wakati nataka kuzungumza naye”Β
“Kwahiyo ukidharauliwa ndiyo umpige Mtu, adabu ya wapi hiyoΒ wewe Kijana, hujui kama upo nyumbani kwa Neema, tena siyo tuΒ kwa Neema bali Mimi nikiwepo alafu unampiga?” Neema akawaΒ anajilizaΒ
“Mama nataka kujua Matilda yupo wapi” Akauliza James
“Matilda, ndiyo Nani…si nakuuliza wewe huyo Matilda niΒ Nani?” akahoji Mama NeemaΒ
“Ni Mwanamke niliyezaa naye, Neema anajua yupo wapi!”Β
“Hivi wewe una utimamu wa akili, yaani Mwanamke uzae nayeΒ wewe alafu uje umtafute kwa Neema, Dunia itakushangaa kwaΒ uzuzu wako, kama Matajiri wote Duniani wana akili kama yakoΒ basi kua na pesa siyo kua na heshima, alafu si ulisema hunaΒ Mtoto, leo unakubali kua una Mtoto tena umekuja kwa NeemaΒ kumtafuta Uliyezaa naye” Akasema Mama yake Neema, James akawaΒ mpole na mwenye kunywea, Mama Neema akamshika mkono NeemaΒ kisha akaingia naye ndaniΒ
“Simtaki huyo Mtu, tafadhali muondoe” Mama Neema akatoaΒ maagizo kwa Mlinzi. James akaingia kwenye gari kishaΒ akaondoka, Baada ya kusikia kua James ameondoka…NeemaΒ akamwambia Mama yake kama si yeye aliyekua akijilizaΒ
“Mama umemyoosha sana”Β
“Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kileΒ sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufungukaΒ kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo MsichanaΒ Mshikilie hadi mwisho.”Β
“Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno”Β
“Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena”Β
“Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatuΒ kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,Β akaingia Mwanaume mmoja..
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
Β
12 Comments
Jamani, mbona inahuzunisha
Ni hataree
β³umetisha xaba
Mtunzi upo vzr unajua kugusa hisia za watu
Aloooohππ
Tamu ial fupi sana jamani
π¨π¨π¨π¨
Upo vzur san
Daaah maskini akipata matako hulia mbwata mbwata mbwata π
Patra kufa cjapendaπͺ
Nimeipendq coz
inatufundisha sanaaa
q989sy