Ilipoishia “James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni Mtotoย wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”ย alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibuย walishtukaย
“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanyaย kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni Mtotoย wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyoย vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”ย alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua naย hasira sana.ย
Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, Mamaย Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakiniย ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James nayeย aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,ย aliondoa gari haraka sana.ย Endeleaย
SEHEMU YA TATU
Mama Naomi akamkimbilia Matilda kujua kwanini James alifikiaย uamuzi wa kumpiga, hakuna alichokizungumza Matilda sababuย bado alikua akilia kutokana na kilichotokea, Mwanaumeย aliyesababisha akatoroka kwao, akawapa Mawazo wazazi wakeย aliishia kumpiga na siyo kujali hali ya Mtoto kisa tu ulemavuย
“Matilda usilie hebu nieleze kimetokea nini hadi akakupiga?”ย aliuliza Mama Naomiย
“Niache Mama Naomi, ilipofikia nimechoka na mateso ya hiiย Dunia ni bora hata nife tu” Alisema kwa hasira Sana Matildaย huku akilia kwa uchungu sana.
“Huo ni uamuzi wa kijinga sana Matilda, ukifa Patra atazidiย kuteseka, angalia jinsi anavyoteseka sasa hivi je ukifaย itakuwaje?”ย
“Sasa nitakaa nikimwangalia Binti yangu akifa mbele ya machoย yangu alafu Baba yake akiwa na uwezo wa kumsaidia lakiniย hafanyi hivyo, ni bora kufa kuliko kumwangalia Patra akifa”ย Alisema Matilda.ย
“Nakuomba Matilda kwasasa turudi nyumbani tutafakari jinsi yaย kuipata pesa ya Matibabu, hebu nyanyuka” Mama Naomiย alimnyanyua Matilda kisha aliondoka naye.ย
********ย
“Mimi nina wao wazo Matilda, kwanini usiende kanisani kwenuย ukaomba Msaada kwa waumini wakakusaidia?” alisema Mama Naomi,ย yalipita Masaa matatu baada ya kurejea nyumbaniย
“Wataweza nisaidia kweli?”ย
“Ndiyo nina imani kubwa watakusaidia sababu wewe ni Muuminiย mwenzao”ย
Ushauri wa Mama Naomi aliufanyia kazi, jioni ilipoingiaย alienda kanisani, wengi walimshangaa maana baada yaย kujifungua hakuonekana tena kanisani, aliofahamiana naoย walikua wakimuuliza jinsia ya Mtoto, Maswali ya kuhusu Mtotoย yalizidi kumfanya Matilda ajisikie vibaya sana.ย
“Mbona unalia?” aliuliza Mchungaji mara baada ya Matildaย kufika ofisini kwa mchungaji wa kanisaย
“Mchungaji Mtoto wangu” Alisema Matilda, Mchungaji alishtukaย akamuulizaย
“Mtoto wako amefanyaje?”ย
“Mchungaji Mtoto wangu Mimi” Sauti ya kilio ya Matildaย ilisikikika na kumfanya Mchungaji aingiwe na maswali mengiย kichwaniย
“Matilda Mtoto wako amefanya nini, hebu punguza kuliaย uniambie” Alisema Mchungaji kwa sauti iliyojaa upole wa Haliย ya juu sana, kwikwi ilimshika sana Matilda kila alipotakaย kusema alijikuta akishindwa, kilio kilimuandama katika kilaย neno alilohitaji kuzungumza, Mtandio wake aliutumia kufutaย chozi lililomiminika kwa wingi, moyo wake ulijawa na simanziย ya hali ya juu sana.ย
“Matilda tambua unanichanganya sana Mimi, sielewi hata niniย unataka kuzungumza. Nakuomba acha kulia sababu ukilia Mimiย siwezi kujua kilichokusibu” Alisema tena Mchungaji wakati huoย Matilda akiwa ameegemea Meza akiwa analia, hata Mchungajiย alilengwa na Mchozi kwa jinsi ambavyo Matilda alikua akiliaย kwa uchungu, dakika tano zilikatika Matilda akishindwa kusemaย chochoteย
“Unasikia Matilda, kua na imani hakuna kinachomshinda Munguย aliye hai, nijuze Mimi ili tujue tunakusaidiaย ย
vipi….Unasikia….” Mchungaji alirudia kumbembelezaย Matilda, angalau kilio kilianza kupunguaย
“Na hapo shavuni umekumbwa na nini?” Aliuliza Mchungaji,ย shavuni Matilda alikua na alama ya kofi alilopigwa na Jamesย kule Hospitalini.ย
“Mchungaji napitia wakati Mgumu sana katika Maisha yangu,ย Mtoto wangu yupo Hospitalini..” Matilda alijikaza akazungumzaย
“Ulipotea kanisani kila Mtu akawa anajiuliza upo wapiย Matilda, kumbe ulijifungua….Enhee nini kinamsumbua Mtotoย wako?” Aliuliza Mchungaji ambaye alionekana kua na umriย mkubwa, ngozi nyeusi na mvi iliyokolea vizuri kichwani, akiwaย amevalia mavazi ya kanisa na msalaba mkononi.ย
“Mtoto wangu ni Mlemavu, anasumbuliwa na Mapafu, anahitajikaย kufanyiwa upasuaji na kibaya zaidi Baba yake Amemkana”ย Alisema Matilda, kilio kilianza upya baada ya kumalizaย kumuelewesha Mchungaji ambaye alishikwa na butwaa, Matildaย alikua Muumini wa kabisa hilo sababu hata kwao alikotokaย alikua Binti wa kanisa hivyo alivyofika Dar alijiunga naย kanisa pia.ย
“Yesu kristo! pole Binti yangu Matilda, hakuna linalomshindaย Mungu wetu aliye hai, yeye halali kwa ajili yetu, Mtoto yupoย Hospitali gani?”ย
“JM Hospital, inahitajika Milioni nane aweze kufanyiwaย upasuaji, hapa nilipo sina hata senti tano na kadiri sikuย zinavyozidi kwenda tumaini la Binti yangu kua hai linazidiย kupotea” Alisema Matilda akizidi kulia kaa uchungu sana.ย
“Twende kwanza Hospitali kwa ajili ya maombi, baada ya hapoย kanisa litaangalia utaratibu wa kukusaidia” Alisema Mchungajiย akiwa ameshasimama,
“Asante Mchungaji George” Alisema Matilda, waliondoka hapoย kanisani kuelekea Magomeni Mapipa ilipo Hospitali ya JM,ย waliondoka kwa gari maalum ya kanisa, Wakiwa barabaraniย Mchungaji alimwambia Matildaย
“Hili jambo litaisha kwa namna nzuri Matilda, kua na imaniย thabiti usitetereke. Kupitia Mtihani huu shetani anawezaย akajipenyeza na kukuingiza kubaya zaidi endapoย hautojiimarisha kiimani” Matilda aliitikia kwa kichwa kishaย alijishika tama.ย
********ย
“Una uhakika?” lilikua ni swali aliloulizwa Neema, alikuaย kituo cha polisi.ย
“Ndiyo sababu yeye ndiye anayeishi pale” alisema Neema kwaย kujiamini kisha akatoa kitita kidogo cha pesa kwa siri sana,ย Polisi akatabasamu sababu ilikua ni ishara kua alichokuaย akikizungumza Neema kilihitaji kutengenezwa zaidi ili kiweย kikubwa.ย
“Jina lako?” Aliuliza Polisi akiwa anaandika jalada la kesi “Neema Ngushi, Miaka 32”ย
“Mshtakiwa?”ย
“Matilda John, Miaka 28” Alisema Neemaย
“Vitu vilivyopotea vina thamani gani?”ย
“Milioni 16” Alisema tena Neemaย
Baada ya kumaliza kuandika maelezo marefu aliyoyatoa, alipewaย RB ya kumkamata Matilda, alichofanya Neema ni kwendaย kumfungulia kesi ya upotevu wa vitu kwenye nyumba anayoishiย Matilda, hakutaka kuendelea kumwona Matilda katika Maishaย yake, pembeni alikua amesimama Mwanaume mmoja ambaye kaziย yake ilikua ni kutingisha kichwa tu.ย
Alipohakikisha amemfungulia kesi, walitoka na Mwanaume huyoย wakaingia kwenye gari, wakaondoka kituo cha polisi.ย
“Unajua huyu Mwanamke anaweza kua kikwazo kikubwa sababuย James alikiri kua Mtoto ni wake lakini anaona aibu kuleaย Mtoto ambaye ni kiwete, sasa hofu yangu ni kwamba akili yaย Matilda ikifunguka alalfu akaenda kudai haki, huwenda Jamesย akajirudi kwake sababu atatakiwa kumtunza Mtoto kwa lazima naย pengine akachukuliwa hatua za kisheria alafu Mimiย nikahangaika” Alisema Neema akiwa anaendesha gariย
“Hapo usiwe na huruma hakikisha unamsotesha hadi akili imkaeย sawa, James akijua itakuaje?”ย
“Hata akijua hawezi kufanya chochote sababu nimeshamwambiaย kua nataka nitengeneze mchezo ili Matilda akubali kurudi kwaoย Njombe” Alisema Neemaย
“Bingoo!!! Sasa tunaenda wapi?”ย
“Naenda kukuacha kwako Sadam alafu Mimi nirudi nyumbani,ย kesho tunamkamata Matilda, naamini kitisho hiki kitamfanyaย akubali kurudi kwao”ย
“Umetisha sana hakika wewe ni jembe la kujivunia Neema”ย Alisema Mwanaume huyo kisha akaweka Mkono wake kwenye paja laย Neema ambaye alikua na Ujauzito wa Miezi mitatu tu.ย
*****ย
Saa 12 Jioni, Gari ya kanisa ilikua ikiingia kwenye geti laย Hospitali ya JM Magomeni Mapipa, Matilda alikua amelia sanaย hadi macho yalimvimba, wakashuka na kuelekea Nje ya chumbaย ambacho Patra alikua amelazwa, Macho ya Mchungaji na Macho yaย Matilda yaligongana na macho ya Daktari ambaye alikua akitokaย ndani ya Chumba hicho.ย
“Dokta samahani hali ya Mwanangu inaendeleaje?” aliulizaย Matilda kwa presha.ย
“Matilda Mtoto anaendelea vizuri kwasasa, aliamka kishaย akalala hadi sasa hivi”ย
“Tunaweza kumwona?”ย
“Ndiyo lakini hampaswi kumsumbua” Alisema Dokta akiwaย anaondokaย
“Asante Dokta, Mchungaji twende” Alisema Matilda kishaย alifungua mlango wa chumba hichoย
“Mwanangu!!” Alisema Matilda baada ya kumwona Binti yakeย akiwa anapumulia Mashine, Roho ilimuuma sana.
“Oooh Jesus” Alisema Mchungaji, Chozi likaanza kumbubujikaย tena Matilda, alikua Mtu wa kulia kila dakika kwa namnaย ambavyo hali ya Binti yake ilikua, Mchungaji akamwambiaย Matildaย
“Kulia hakusaidii chochote, ngoja tufanye kwanza Maombi iliย tumkabidhi Mtoto huyu na hali yake mbele za Mungu” Alisemaย Mchungaji Georgeย
Alianza kufanya Maombezi kwa Mtoto Patra, aliomba kwa imaniย kubwa sana, Matilda naye alizama kwenye Maombi akisaidiana naย Mchungaji huyo, maombi yalifanyika kwa sauti ya chini sanaย ili wasimsumbue Mtoto kama ambavyo Daktari alikua amewaambia.ย Zilitumika dakika arobaini na tano hadi kumaliza kumwombeaย Patra, Jasho lilikua likimvuja Mchungaji huyo ambaye kilaย alivyomwangalia Patra alijiskia vibaya sana kwa jinsi hli yaย Mtoto huyo ilivyokua.ย
“Mungu amepokea Maombi Matilda, anaenda kutenda kwa ajiliย yako na Mtoto, atafungua minyororo ya mateso kwa Mtoto huyu,ย amini kua amekwisha kombolewa” Ilikua ni kauli ya kutia moyoย ya Mchungaji huyo ambaye alikua amemshika bega Matilda, maraย aliingia Daktari akawaambia Muda umeisha.ย
“Baby leo nimefanya kitu ambacho kitakuondolea hasira sana”ย Alisema Neema akiwa anakula embe bichi, alikua akimwambiaย James wakiwa chumbani Usiku.ย
“Jambo gani hilo?”ย
“Ni kuhusu Matilda”ย
“Sitaki hata kumsikia huyo Mwanamke Neema, katika Maishaย yangu sijawahi pata ona Mwanamke King’ang’anizi kama Matilda”ย Alisema kwa hasira James, alionesha wazi hataki kusikiaย kuhusu Matilda ambaye alitoka kumpiga Kule Hospitalini.ย
“Usikasirike sababu hili jambo litaenda kumfanya aondoke hapaย Dar bila kupenda Bby”ย
“Nakusikiliza”ย
“Hii hapa ni RB ya kumkamata kwa kosa la wizi wa vitu kwenyeย ile nyumba, naamini akilala polisi siku moja akili itamkaaย sawa” Alisema Neema kisha alimpatia Karatasi kutoka polisi,ย James akaisoma kwanza kabla ya kusema Chochote, kishaย akamtazama Neema
“Umemfungulia kesi?”ย
“Ndiyo!! lengo langu apate kitisho kitakachomfanya aiyone Darย chungu, nimefanya hivyo sababu sitaki kumwona Baba Mtotoย wangu mtarajiwa anakosa raha” Alisema Neema, Jamesย alitabasamu sababu aliitwa Baba Mtoto, alihitaji sana Mtotoย
“Mbinu yako ni bora sana Neema, naamini kwenye hiliย hachomoki, ataondoka hapa Dar atake asitake, tena kwa kuondoaย kero nitampatia na pesa ya kuanzia Maisha huko aendapo”ย Alisema James kwa furahaย
“Umeona jinsi gani nakupenda, nakuhitaji na pia nakuthamini,ย furaha yako ndiyo furaha yangu Mpenzi” Alisema Neemaย akiendelea kula embe kwa chumvi.ย
Neema alishajua udhaifu wa James, wala hakutumia nguvu nyingiย kumfanya James afurahi, ni kumweleza tu kuhusu ujauzito,ย alichotaka alipewa bila hata kulazimisha.ย
Siku iliyofuata, Neema alienda kituo cha polisi akaonana naย yule polisi ambaye aliandika jarada la kesi ya Matilda,ย akaomba askari kwa ajili ya kwenda kumkamata Matilda, akapewaย askari polisi wawili akaenda nao moja kwa moja JM Hospital.ย
Muda huo Matilda alikua kanisani, zoezi la kukusanya pesa kwaย ajili ya kuratibu matibabu ya Patra lilikua likiendeleaย kanisani hapo chini ya uangalizi wa karibu wa Mchungajiย George ambayo alimwambia Matilda kua atasimama naye bega kwaย bega hadi Patra apone, Mama Naomi alikua miongoni mwa Watuย waliofika kanisani hapo baada ya kupewa taarifa na Matildaย kua litaendeshwa zoezi la Uchangiaji wa matibabu ya Patra.ย
Chozi halikuacha kutoka kwenye macho ya Matilda baada yaย kuona uchangwaji wa pesa hiyo, muitikio ulikua mkubwa sanaย kiasi cha kumtia moyo hata Mchungaji wa kanisa hilo ambaye niย Mchungaji George. Nyimbo za kusifu zilikua zikiimbwa, kilaย mwenye kua nacho alitoa kidogo alicho nacho kwa moyo woteย bila kujaliย
Waumini waliungana kwa pamoja ili kurejesha furaha ya Matildaย ambaye alikua haamini macho yake jinsi kapu lilivyokuaย linajaa noti. Mikono ya Matilda ilikua kwenye mdomo wake hukuย chozi likiendelea kuvuja, tabasamu pana lilionekana kwenyeย sura ya Mama Naomi ambaye alitoa wazo la Matilda kurejeaย kanisani. Mchungaji George alimtia moyo sana Matilda katikaย kila hatua ambayo walikuwepo, baadaye Mchungaji alikabidhiwaย kapu lenye fedha hizo.
Watu maalum wa kuzihesabu walianza kazi hiyo huku Mchungajiย George akitoa neno kanisani hapoย
“Hakika leo Bwana ameinuliwa, kwa moyo huu uliooneshwa hakikaย roho mtakatifu yupo ndani yetu, kusimama na Mwenye matatizoย kunaongeza Baraka, hamjui ni kiasi gani Mungu anaendaย kuongeza kilichopungua kwenu. Mungu awabariki sana kwa jinaย la yesu” Alisema Mchungaji huku kanisa likiitika haswa kwaย kusemaย
“Aaameen” Matilda alizidi kulia kwa uchungu sana,ย kilichomliza siyo tu kuumwa kwa Binti yake bali ni maishaย anayopitia baada ya kuitwa Mama, jinsi watu bakiย wanavyosimama na yeye wakati Mwanaume aliyemfanya akatorokaย kwao hajigusi kwa lolote lile, alipiga magoti na kusemaย
“Asante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja naย kumwinuaย
“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji Georgeย alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti.ย Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umatiย ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa Matildaย Msichana wa miaka 28ย
Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikuaย kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpaย ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisaniย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
10 Comments
Daaaah jmn
Kama naangalia tamthia vileee๐ญ๐ญ
Wakati wa Mungu ukifika Kila lililoshindikana litafanyika kwani hakuna jambo gumu kwake
Mungu hakosei kwakweli
Mambo Yazidi kuwa motooo
God’s ears are not deaf that he cannot hear your ๐ญ cry ..
Kuna funzo apa
Mamb ni moto
Am I crying too ๐ญ
Daah pole san kam wap
ge6l84