“Ahsante Mama Naomi” Ilikuwa ni sauti yenye upole, MatildaΒ alikuwa akimwambia Mama Naomi huku chozi likimlengaΒ
“Usijali Mdogo wangu Maisha ndivyo yalivyo, ni wajibu wanguΒ kukusaidia” Alisema Mama Naomi akiwa amesimama Mlangoni,Β alikuwa amempatia Matilda kiasi cha shilingi Elfu tanoΒ
“Nashukuru sana, Mungu azidi kukupa Mama Naomi, unaweza onaΒ hili ni dogo kwangu lakini Ulichonifanyia ni kikubwa mno”Β Alisema Matilda akiwa analia, chozi lilimlenga Mama NaomiΒ akamwambia MatildaΒ
“Mpeleke Mtoto Hospitalini Matilda, utanijulishaΒ kitakachoendelea” Alisema Mama NaomiΒ
“Ahsante sana ngoja niwahi” Akasema Matilda kisha akakimbiaΒ haraka kurudi anakoishi. Usiku huo ambao ulijawa na giza neneΒ Matilda alikatiza Uchochoro ili awahi kufikaΒ
Bahati mbaya akakutana na vibaka wakampora pesa na kumpigaΒ
“Jamani pesa ya Mwanangu hiyo nawaombaa, Nisaidieni Jamani”Β Aligumia Matilda lakini vibaka hao walikimbia, MasikiniΒ alilia sana Matilda, alikuwa Msichana wa Miaka 26 tu, akarudiΒ anakoishi akiwa mnyonge mno, akaingia hadi nyumbani kwake,Β akamtazama Mtoto wake aliyeitwa Patra, alikuwa mgonjwa kwaΒ zaidi ya miezi mitano akiwa ni Mtu wa kulala na kulishwa,Β Mtoto huyo alikuwa na miaka mitatuΒ
Chozi likamvuja Matrida, alimtazama Patra akashindwaΒ kuvumilia akakimbilia nje na kuanza kulia.Β
Asubuhi Mapema, Mama Naomi alikuwa wa kwanza kwenda nyumbaniΒ kwa Matilda, akamkuta akiwa amevimba macho kwa kulia
“Mbona unalia Matilda?” aliuliza, alikuwa kama ameongezaΒ kilio kwa Matilda, alizidi kulia kwa uchungu sanaΒ
“Usilie Matilda, Mitihani ndiyo nguzo muhimu kwenye MaishaΒ yetu sisi wanadamu, vipi ulifanikiwa kwenda Hospitali?”Β aliuliza Mama Naomi akiwa amebeba deli la kuuzia vitumbuaΒ
“Usiku ule nilikabwa na kuibiwa pesa Mama Naomi, hicho ndichoΒ kinachoniumiza, laiti kama ningelijua kuwa pesa ile ingeibiwaΒ ni bora ningekuachia ikusaidie mwenyewe” Alisema kwa UchunguΒ sana MatildaΒ
“Masikini pole Mdogo wangu, Eeeh Dunia yako ina mitihaniΒ mingi lakini Usijali Mdogo wangu sawa?”Β
“Sawa Dada, leo sina pesa ya kula ila Mungu ndiyo anajuaΒ nitaishi vipi na huyu Mtoto, afadhali ningekuwa mwenyewe MamaΒ Naomi yaani kila nikimtazama Patra nazidi kuumia” AlisemaΒ Matilda akiwa analia, Chozi lilikuwa likimvujaΒ
“Usijali, Basi chukua hii hapa itakusaidia, nikirudi tutaonaΒ jinsi ya kumpeleka Hospitali Patra” Alisema Mama Naomi, japoΒ naye alikuwa masikini lakini aliguswa mno na Maisha yaΒ MatildaΒ
“Sitaki kuwa mzigo kwako Dada, sipokei pesa yako sababu hataΒ wewe kula yako ya shida, acha Mungu anipiganie Mama Naomi”Β
“Usiseme hivyo, Mtoto anatakiwa kula ili ameze dawa Mtilda,Β sifanyi kwa ajili yako bali kwa ajili ya Mtoto wako Patra”Β Alisema Mama Naomi, akampatia elfu mbili Matilda kishaΒ akaondoka. Alipofika nje aligeuka na kuitazama nyumbaΒ anayoishi MatildaΒ
Alikuwa akiishi kwenye nyumba nzuri sana ambayo laiti kamaΒ ungeambiwa kuwa anakosa hata shilingi Mia ya kununua panadolΒ huwezi aminiΒ
“Eeeh Mungu mpunguzie Mitihani Matilda, anateseka sana”Β Akajisemea kisha akaondoka zakeΒ
Mara honi ya gari ikasikika, Matilda akajiuliza ni NaniΒ aliyekuja, akaenda getini kuangalia, alishangaa kidogo kishaΒ akafungua geti, likaingia gari la Kifahari sana, baada yaΒ kuegesha akashuka Mwanaume mmoja akiwa na MwanamkeΒ Β
“James afadhali hata nimekuona, Mtoto hali yake si nzuri sikuΒ ya tatu sasa kula ni shida, anahitaji matibabu” AlisemaΒ MatridaΒ
“Sasa unaniambia Mimi kama Nani?” aliuliza huyo James “Wewe ni Baba wa Mtoto wangu James” Alisema MatildaΒ
“Oooh kumbe…sikujua kama ni Baba, eti nina Mtoto mwenzio”Β Alisema kwa utani kisha akacheka na Mwanamke aliyekuja naye,Β akampiga busuΒ
“Sikia Matilda, nilikwambia unizalie Mtoto na siyo Mfu, yuleΒ siyo Mtoto niliyekuwa namtaka, unawezaje kuwa na ujasiri waΒ kuniita Baba wa Mtoto ambaye ni zezeta? hivi unanionaje kwaΒ mfano, nilivyo naweza kuwa na kitoto kama kile?” alisemaΒ James kisha akashika tumbo la huyo Mwanamke aliyekuja nayeΒ
“Mtoto wangu yupo humu Matilda, tafuta Baba haraka sana waΒ hiyo maiti iliyo ndani, hautokuwa na muda mrefu wa kuendeleaΒ kuishi hapa kwani Neema akijifungua atakuja kuishi hapa naΒ Mtoto wangu. Ila usijali sababu mimba bado changa hivyo unaΒ miezi tisa ya kulea maiti yako” Alisema James, chozi lilizidiΒ kumvuja Matilda, maneno ya kikatili yalimuumiza sanaΒ
“Baby hii ndiyo nyumba yako, utaishi hapa baada ya kujifunguaΒ sawa?” alisema JamesΒ
“Asante Baby….sitaitwa Neema tena bali Mama fulani….”Β Alisema huyo Mwanamke wakiwa wanachekaΒ
“ila Baby mpe hata pesa kiduchu apate kula maana anaonekanaΒ mdhaifu sana” Alisema NeemaΒ
“Kwakuwa umesema wewe Baby basi nitampatia” Alisema JamesΒ kisha akatoa noti ya elfu kumi akamtupia Matilda, JamesΒ alikuwa ni Mwanaume mtanashati sana, akaingia kwenye gari naΒ Mwanamke wake wakaondoka hapo.Β Β
Matilda akainama na kuokota noti hiyo japo ilitolewa kwaΒ masimango lakini ilikuwa ni pesa muhimu sana kuendesha MaishaΒ yake, akafunga geti kisha akarejea ndani, akatulia kochiniΒ akiwa anakumbuka jinsi alivyokutana na JamesΒ
Njombe Tanzania, Baba yake Matilda alikuwa ameketi na MamaΒ yake Matilda nje ya nyumba yao, Baba Matilda akamuuliza MamaΒ MatildaΒ
“Hatuna sababu ya kuendelea kuamini kuwa Matilda yupo haiΒ sababu ni muda mrefu tangu alipotoweka, hatuna taarifa zakeΒ na hatujui huko aliko kama yupo hai au amekufa, kwaniniΒ tusiweke Msiba?” alihoji akiwa ameketi, Mama MatildaΒ akajaribu kumsihiΒ
“Hatuwezi kufanya hivyo hadi pale tutakapo pata uhakika kuwaΒ Matilda amekufa, hisia zangu zinaniambia kuwa MatildaΒ anaishi” Alisema Mama Matilda kwa Uchungu sanaΒ
“Bado unaamini hivyo hadi leo?”Β
“Ndiyo Baba Matilda, tumuombee Binti yetu popote alipo MunguΒ anyooshe mkono wake arejee nyumbani” Alisema Mama yakeΒ Matilda, ilikuwa ni familia yenye majonzi baada ya MatildaΒ kutoroka hapo, hakuna aliyejua kuwa Matilda alikuwa hai naΒ alikuwa akiishi Dar tena kwa mateso makubwa sana.Β
“Nimesikia Maimuna anaelekea Mjini kesho, naenda kumwelezaΒ kuwa kwa upande wake ajitahidi kumtafuta Matilda huwendaΒ alitorokea Mjini” Alisema Mama Matilda ambaye alionesha kuwaΒ hayuko tayari kuamini kuwa Binti yake amekufaΒ
“Sawa! siku ukikata tamaa utanieleza tuweke Msiba” AlisemaΒ Baba Yake Matilda, Basi Mama Matilda akaelekea kwa Maimuna.Β
Familia ilimkumbuka sana Matilda ambaye alitoroka kwao NjombeΒ na kwenda kuishi Dar, yote aliyokuwa anayapitia hakunaΒ aliyekuwa akiyajua kabisa, Maimuna alipewa kazi ya kumtafutaΒ Matilda Njombe Mjini bila kujua kuwa Matilda alikuwa Dar.Β
Usiku ulipoingia, Matilda alisali ili Mungu ampe unafuu waΒ Maisha, alipomaliza aliketi kisha akamwambia Binti yakeΒ aliyekuwa kitandani akiwa hawezi kutingisha japo kidoleΒ
“Patra Mwanangu muda siyo mrefu utakuwa sawa, Mungu haweziΒ kutuacha kirahisi tukaangamia” Alisema Huku choziΒ likimbubujika. Maisha ya Matilda yalijaa maumivu makali sana,Β Mara geti liligongwaΒ
Akaenda kufungua akakutana na Mama Naomi ambaye alikuwaΒ amebeba chakula kwenye HotpotΒ
“Jitahidi ule na Mtoto” Alisema Mama Naomi
“Nashukuru sana Mama Naomi na Mungu akubariki” AlisemaΒ Matilda kisha alipokea chakula kutoka kwa Mama NaomiΒ
“Msalimie shoga yangu Patra Mie hata siingii, nimemuachaΒ Naomi anakula” AlisemaΒ
“Haya Lakini Ahsante sana”Β
“Usijali Matilda, nakutakia Usiku mwema” Alisema Mama Naomi,Β Matilda alishukuru tena kabla ya Mama Naomi kuondoka.Β
Aliporudi sebleni aliketi kisha akawakumbuka wazazi wakeΒ aliowaacha NjombeΒ
“Siwezi kurudi Njombe, Baba na Mama mimi nipo hai napiganiaΒ Maisha yangu” Akasema maana naye alijua ni jinsi gani wazaziΒ wake walikuwa wakihangaika kumtafutaΒ
Siku iliyofuata hali ya Patra ilibadilika akawa anahema kwaΒ shida sana, Matilda akakimbilia kwa Mama Naomi akamueleza,Β wakarudi pamoja na kumchukua Patra hadi HospitaliniΒ
Baada ya vipimo dokta akawaambia kuwa Mtoto anatakiwaΒ kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kusafisha mapafu yake,Β kuanzia muda huo Patra akawekwa kwenye chumba maalum hukuΒ akisaidiwa na Mashine ya kupumuliaΒ
“Upasuaji ni gharama Dokta, Nami sina uwezo wa kugharamia!”Β Alisema MatildaΒ
“Itabidi uhangaike Dada yangu sababu bila hivyo utampotezaΒ Mtoto, fanya uwezavyo hakikisha unapata kiasi cha shilingiΒ milioni 8 ili kunusuru Maisha ya Mtoto” AlisemaΒ
“Dokta kama alivyosema hali ya Maisha imezidi kuwa ngumu,Β hakuna namna Hospitali inaweza ikatusaidia ili kuokoa MaishaΒ ya Patra?” Alidakia Mama NaomiΒ
“Yote hayo yameangaliwa kwa mapama na marefu yake, HospitaliΒ inaweza kukusaidia ila mzunguko wake ni mrefu mno kiasiΒ kwamba itahatarisha hata Maisha ya Mtoto, wewe hangaikaΒ utakapofikia utasema” alieleza DoktaΒ
Mama Naomi na Matilda wakatoka hapo, Mama Naomi akiwa naΒ Mtoto Mgongoni akamueleza Matilda
“Itabidi uwende kwa James akakusaidie maana hicho kiasi niΒ kidogo kwake”Β
“Mama Naomi, James amemkataa Mtoto mara baada ya kuzaliwa tu,Β hawezi kugharamia chochote licha ya kuwa Mimi najua Mtoto niΒ wake” Alisema MatildaΒ
“Damu ni nzito kuliko Maji, hebu piga moyo konde twendeΒ tukajaribu” Alisema Mama NaomiΒ
“Haya twende Mama Naomi japo Moyo wangu unasita kwenda kwaΒ James, unajua James wakati ananitongoza aliniambia anahitajiΒ Mtoto, kama nitamzalia atanipa nusu ya Mali zake lakiniΒ alibadilika baada tu ya kujifungua”Β
“Yaliyopita si ndwele Matilda hebu twende kwa James,Β alivyolala jana sivyo alivyoamka leo” Mama Naomi alizidiΒ kumpa tumaini Matilda hadi akakubali kwenda kwa JamesΒ kumweleza kuhusu MtotoΒ
Mishale ya saa tano wakapanda Daladala kuelekea Sinza moriΒ kutokea Hospitali ya JM iliyopo Magomeni mapipa, KwenyeΒ daladala Matilda alikuwa kimya sana akitafakari ni jinsi ganiΒ atamueleza James, Mwanaume ambaye alionesha chuki na hasiraΒ dhidi yake pindi tu alipojifungua Mtoto mlemavu, lakiniΒ ilikuwa ni lazima akaonane na James ili asaidiwe pesa yaΒ matibabu ya Mtoto. Alikua amekaa siti ya mbele karibu naΒ dereva huku akipikicha macho yake kuzuia chozi kuvuja maanaΒ moyo wake ulijaa maumivu makali mno kila alipofikiria kuhusuΒ Mtoto wake.
Haikuchukua muda mrefu wakafika Sinza ambako ofisi ya JamesΒ ilikuwepo, alikuwa hapafahamu mahali ambapo James alikuwaΒ akiishi isipokua ni kazini kwake, akasali kidogo kabla yaΒ kugonga mlango.Β
Mlango ukafunguliwa na Mdada mmoja, akawaona Matilda na MamaΒ NaomiΒ
“Karibuni, sijui niwasiadie nini?” Aliuliza Mdada huyo mwenyeΒ rasta asiliaΒ
“Asante, Tunashida na James” alisema MatildaΒ
“Mmeongea naye kuwa mnakuja? Maana ametoka muda siyo mrefu” “Oooh ameeleekea wapi?” Aliuliza Matilda
“Nahisi atakuwa anaelekea kwake maana mara nyingi huwaΒ akitoka harudi hadi kesho yake”Β
“Sawa Asante”Β
“Haya karibuni tena” Alisema huyo Mdada, kisha alifungaΒ mlango, Mama Naomi na Matilda walitazamana maana majibuΒ waliyasikia kwa panoja, chozi lilimlenga MatildaΒ
“Usijali Matilda tusikate tamaa kwani kwa kufanya hivyoΒ hatutoweza kumsaidia Patra, cha msingi ni kumtafuta James,Β hebu mpigie nitaongea naye”Β
“Haya”Β
Matilda akatoa simu na kumpigia James lakini simuΒ haikupokelewa kabisa, Matilda alikaa chini akaanza kulia kwaΒ uchunguΒ
“Matilda hapa ni ofisini kwa Watu, nyanyuka turudiΒ Hospitalini, tutamtafuta wakati mwingine sawa!!”Β
“Lakini mwanangu Mama Naomi, kwanini Mimi tu kila siku,Β nimemkosea nini Mungu?” Alisema kwa sauti iliyojaa kilioΒ
“Hakuna ulichomkosea Mungu Matilda, yeye anapanga naΒ kutekeleza, hii ni mitihani yake, hakuna kilioΒ kinachodumu….yataisha tu haya nyanyuka” Maneno ya busara yaΒ Mama Naomi yalimsukuma Matilda akaamka, wakaanza kuondokaΒ kurudi Magomeni mapipa.Β
Walipofika Hospitalini Magomeni Mapipa, Mama Naomi alimuagaΒ Matilda sababu alikuwa na Mtoto mdogo, alihitaji kwendaΒ nyumbani lakini alimtaka Matilda kuwa jasiri sababu akiliaΒ haitosaidia chochote kile.Β
“Asante Mama Naomi, Mungu azidi kukubariki” Alisema Matilda ******Β
“James una hakika kuwa hii ni Mimba yako?” Lilikua ni swaliΒ aliloulizwa James, walikuwa chemba na Mama yake wakimuachaΒ Neema akiwa sebleniΒ
“Ndiyo Mama kwanini unauliza hivyo?” Alihoji James akiwaΒ anamtazama Mama yake, alikua ameenda kumtambulisha Neema kwaΒ Mama yake huko KiwalaniΒ
“Nimekuuliza tu sababu imekuwa ghafla sana James” Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Pili Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
31 Comments
wa kwanza dadeki zangu
Daaaa patamu hapo james atalia baadae
Mwanzo tu shughuli inaonekana
Aiseeeee
Malipo ni hapa hapa duniani
Nzuri
Daaah mbn chozi linanitoka huku ni sehem ya kwanza π€πͺ
Maisha mtiani
Asante mtunzi
Duuuu rwaya tamuuu et
Kwa siku ziwe mbili bas maaana daj
Inabamba.
Ina heat sana safi sana KAKA MKUBWA isiishe haraka
Huyu james namjua mimi
Sana adminπ₯
James umbwaaa
Haya sasa
Hii ni chuma kwa chuma
Hi kali
James atakuj kujuta
Ebwana eeeh James James James nikekita mara tatu
Inatisha hatrii maumiv mwanzo mwishoo
imetulia sana
James mungu atakup unachostahil malip hp hp dunia
Story nzur inafundisha Sana cjui uko mbele itakuaje
Nice
Nanjoi San kila riway hii
Sio poa anacho James kifanyΓ
200u21
rz6mho
y7sthh