Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Chama Clatous Na Kumbukizi Ya Kurasa Za Ajibu
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Chama Clatous Na Kumbukizi Ya Kurasa Za Ajibu

    Living ShayoBy Living ShayoJuly 27, 2024Updated:July 27, 202410 Comments3 Mins Read7K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Clatous Chama
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Wakati ambao Ibrahim Ajibu anaibuliwa na Simba SC ilikuwa ngumu kuamini kuwa anaweza kufanya makubwa na Kiwango bora, lakini jambo kubwa kwa klabu ya Simba SC ni Imani kubwa kwake na kwa vijana wenzake kutoka timu zao za vijana.

    Alidumu kwa muda mrefu sana na Simba SC kiwango bora, ufundi na kujituma kiwanjani, ilifika hatua akaimbwa na mashabiki na wapenzi wengi nchini bila kujali upande wowote ule anaocheza mchezaji huyo.

    Ilifika hatua Ibrahim Ajibu akabatizwa majina yaliyokuwa yanaendana na namna anavyocheza, sikushangaa alipopewa Jina la “Mwamba wa makororo” wengi waliamini kuwa ndiyo mchezaji pekee aliyekuwa na ufundi mwingi nchini kwa kizazi chao.

    Kuna msemo maarufu aliyowahi kuusema kipa wa Simba SC Aish Salum kuwa “Mchezaji bora anachukua mataji”, ukame na ugumu wa kuchukua makombe kwa miaka yake ya ubora ndani ya Simba SC yalimpa hamasa na kuamia upande wa pili kwa ajili ya kuchukua na kubeba makombe.

    Na nikukumbushe kuwa wakati anaondoka Simba SC upande wa pili ulikuwa bora sana na walichukua makombe yote makubwa nchini huku upande wa Mnyama akijitafuta na kuunda kikosi kipya kwa ajili ya kufanya makubwa baada ya muda mrefu na ndiyo wakati ambao waliunda timu bora sana kiwanjani.

    Alipojiunga tu na Yanga SC ni kama aliama na ukame wa makombe aliyokuwa akiyatamani wakati Yanga SC akinyanyua na yeye akiwa upande wa pili, ni kama alipishana na mafanikio na msimu ambao anatangazwa Yanga SC ndiyo msimu ambao Mnyama akanyanyua makombe makubwa nchini, licha ya kiwango bora sana Jangwani ila aliambulia patupu kwa misimu miwili na kuamua kurejea Simba SC na alichukua makombe bila ya kuwa na kiwango bora ambacho alionyesha kabla na baada ya kuondoka unyamani.

    Wacha nikurejeshe tena hapo hapo Simba SC, 2018 walimtambulisha Kiungo Clatous Chama akitokea kwao Zambia huku akiwa Hana Jina na umaarufu wowote ule wa kisoka kwa kiwango kikubwa nchini kwao, ila kikubwa kwa Simba SC ilikuwa ni Imani kwake kama ambavyo walifanya kwa kijana wao mwenyewe waliyemuandaa.

    Ilimchukua msimu mmoja tu kuonyesha ubora wake, watu wa mpira nao wakaanza kumpa jicho la pili na la tatu kuona uhalisia wa kiungo huyo, msimu uliyofuata ni kama Imani ikaanza kulipa ufundi, udambwi udambwi na ubora wa Clatous Chama ukaonekana na hapo ikawa wakati rasmi kwa wapenzi, mashabiki na watu wa kimpira kumuimba Fundi huyo ambaye alikiwasha sana na kuwa tegemezi.

    Utulivu ndiyo ilikuwa silaha yake kiwanjani akili ya kimpira iliambata naye awapo kiwanjani. Ilifika wakati wa kumuheshimisha na jambo kubwa ni kupewa majina mbalimbali ambayo yaliaakisi kile alichokuwa akikifanya kiwanjani.

    Nikuambie tu hata mimi sikushangaa alipoitwa “Mwamba wa Lusaka” au “Brain ya mpira” ni kama mashabiki na wapenzi wa mpira nchini walimbatiza majina ambayo yalikuwa yanaendana na kile mchezaji alichokuwa akikifanya kiwanjani.

    Baada ya muda mrefu wa kuchukua makombe akiwa na Simba SC, ukame ukaanza ndani ya timu hiyo na baada ya muda Kumbukizi ya Ibrahimu Ajibu na Simba SC ikaonekana kwa Clatous Chama, sinema ambayo Ajibu aliifanya Chama naye ameirudia, wakati ambao Ibrahimu anaondoka Simba ilikuwa hawajachukua makombe na wakati ambao Chama anaondoka Simba nao pia wana muda hawajachukua Makombe.

    Akili yangu bado imebaki inawaza na kufikiria kuwa kile kilichotokea kwa Ibrahim Ajibu kinaweza kutokea tena kwa Clatous Chama? Lakini nakumbuka kuwa ubingwa unaamuliwa kiwanjani na baada ya msimu kutamatika tunampata bingwa kati ya wengi. Basi na mimi nikajisemea mwenyewe tu kuwa Wacha niache nafasi na muda utaongea kunipa majibu ya maswali yangu kati ya kurasa hizo mbili tofauti.

    SOMA ZAIDI: Hatukatai Umefanya Vingi Ila Hili Ni Deni Kubwa Sana Kwako

    kaizer chiefs vs yanga usajili wa chama yanga

    10 Comments

    1. Jjb-hsnf-fdk on July 27, 2024 2:17 pm

      Sawa lakn kusema kwamba chama anapishana na makombe hapo sio kweli
      Wakati mwingine haiitaji kukariri na kuamin yaliyopita mim naamin
      Simba kuchukua ubingwa
      Bado sana.

      Reply
    2. Banza JB on July 27, 2024 2:34 pm

      Yanga hii ni Bora
      Simba hii ndio inaanza kujitafuta
      Lolote linawez likatokea

      Reply
    3. Newton on July 27, 2024 2:42 pm

      Endelea kuishi kwa kukariri.

      Reply
    4. Vitalice on July 27, 2024 3:14 pm

      Kikibw tuombe uzima mungu atulinde ligi yetu ianze tujue nn maan ya ubaya ubwela na nyiee hamuogopi

      Reply
    5. Isihaka on July 27, 2024 3:56 pm

      Ukiangalia kwa nadharia unawez ukasem yanaweza chama kumkuta ya ajibu ila mpira haukaririki inawez ikawa tofaut

      Reply
    6. Venance on July 27, 2024 6:30 pm

      Yatatokea na atasugua sana benchi

      Reply
    7. Hatikram on July 28, 2024 8:56 am

      Sema Simba wanatambaa Sana na kikos chao atujakiona

      Reply
    8. Salumu on July 28, 2024 9:54 am

      Mmmmmh inawezekana ngoja tusubili Msimu uanze

      Reply
    9. Ikram baba on July 28, 2024 10:09 am

      Itakuwa inajirudia ya msimu ule ajibu maana chama kakurupuka sana

      Reply
    10. Pingback: Ni Ngumu Kuamini Kamwe Unaondoka Jangwani

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.