Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (08)
    Hadithi

    Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 1, 2024Updated:June 2, 202429 Comments8 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Nyumba Moja Na Majini
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Nilimsimulia kila kitu cha siku ile tu lakini, sikugusia mambo ya nyuma.

    β€œDu! Kwa hiyo mimi nikusaidieje?”

    β€œNaomba tuingie wote ndani, nataka nikachukue simu yangu tu nimpigie huyo jamaa.”

    β€œDa! Itakuwa ngumu kidogo, unajua mimi nina haraka sana leo,” alijitetea yule mtu ambaye kwa umbo ni bonge la mtu. Nilijua ni uoga tu, hakuwa na kuwahi wala kuchelewa “

    Endelea SEHEMU YA NANE (08)

    Alipopita, akatokea mwingine, mzee mmoja, kichwa chote kilichafuka kwa mvi. Nilimsalimia huku nikimwonesha ishara kwamba nataka kuzungumza naye.

    β€œMzee samahani sana.”

    β€œBila samahani kijana.”

    Naye nikamsimulia tukio la siku ile,Β  lakini wakati ananisikiliza, mara nilimwona anatupia macho dirishani na mimi nikageuka kuangalia, sikuona mtu.

    β€œUmeona nini mzee wangu?”

    β€œNimeona msichana ananizomea.”

    β€œKweli?”

    β€œEe. Ndiyo hayo mambo unayosema?”

    β€œNdiyo hayo mzee.”

    β€œTwende,” alisema, nikaanza kutangulia mbele, mzee akanifuatia kwa nyuma. Hatukuwa tukiongea chochote, najua sababu. Kila mmoja alikuwa anaiwaza hatari ya mbele.

    Tuliingia ndani, tukafika sebuleni, lakini sikuiona simu kwenye kochi.

    β€œOna sasa mzee, simu niliitupia hapa, lakini haipo.”

    β€œAu unayo mfukoni kijana?”

    β€œHapana, nina uhakika,” nilisema huku nikijipapasa mifukoni, hakukuwa na simu.

    β€œNitajie namba nijaribu kuibipu,” yule mzee aliniambia huku akitoa simu yake mfukoni. Nilimtajia namba zote, akawa anaziandika, kisha akapiga huku simu akiwa ameiweka kwenye sikio lake la kulia. Nilishtuka sanaΒ  kusikia simu yangu inaita kutokea kwenye chumba cha wale wapangaji wenzangu.

    β€œSi hiyo?” yule mzee aliniambia akiniangalia kwa mshangao.

    Mzee alikata kisha akapiga tena, ikaita tena kutokea kulekule, nilizidi kuogopa, nikamwambia tutoke lakini uzee kweli dawa, aliniambia hakuna haja ya kutoka dawa ni kupambana tu.

    Alinisogelea na kuniambia kwa sauti ya chini:

    β€œNiwagongee mlango?”

    β€œSi watakasirika?”

    β€œSasa kama unaogopa watakasirika, unadhani simu yako utaipataje?”

    β€œHaya wagongee. Lakini subiri, kwa nini tusiende kwanza chumbani tukajua nani alikuwa anachungulia nje?”

    β€œKijana unaonekana muogamuoga sana, we mwanaume bwana, jifunze kukabiliana na hali kama hii, sawa?”

    β€œSawa mzee.”

    β€œHaya twende huko chumbani kwako unakotaka tukaone huyo msichana.”

    Tulifungua mlango wa chumbani, hakukuwa na mtu, ila shuka nililoliacha kitandani asubuhi silo, lilitandikwa jingine pia la kwangu.

    β€œKhaa!” nilishangaa.

    β€œNini?”

    β€œHili shuka.”

    β€œLimefanyaje?”

    β€œSilo nililolitandika asubuhi.”

    β€œLakini la kwako?”

    β€œNdiyo langu.”

    Niliangalia mazingira mengine ya mle ndani na kubaini kwamba, kuna vitu vingi sana vilikuwa ndivyo sivyo.

    β€œSi umeona hayupo?” yule mzee aliniuliza, nikamjibu ndiyo, akasema twende tukachukue simu yetu kwenye kile chumba ambacho ilikuwa inaita.

    Moyo wangu ulikuwa mzito sana, nilihisi kizunguzungu, nilitamani kukaa chini na kumwomba yule mzee asichukue uamuzi wa kuifuata ile simu, lakini ningeipataje simu yangu wakati ina namba kibao?

    β€œKijana, ngoja nikuoneshe dawa moja ya hao viumbe wasiotaka kuonekana,” alisema yule mzee, nikamuuliza ni ipi hiyo.

    β€œTulia wewe,” alisema huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kimfuko kidogo, akakifungua akatoa kitu. Nilipomuuliza ni nini akajibu:

    β€œNi bangi.”

    β€œSawa kabisa, hiyo ndiyo dawa, ngoja nikupe kiberiti.”

    Katika mambo yaliyonishangaza ni hilo, tulitafuta kiberiti chumbani hadi sebuleni lakini hakikuonekana, mbaya zaidi mimi nilikuwa na kawaida ya kununua viberiti bunda zima, lakini pia sikuona popote.

    β€œKweli una kiberiti ndani?” yule mzee aliniuliza.

    β€œKiberiti kipo na uzuri ni kwamba, nina bunda zima, pia silioni.”

    Nilimwona yule mzee akisimama wima na kunyoosha mikono juu kama mtu anayeomba dua kwa Mungu.

    β€œKijana nimejua sasa, ngoja kidogo,” alisema huku akitoka na mimi nikimfuata kwa nyuma.

    Wakati tunapita kwenye korido jirani na vyumba vile vya wenzangu, nikaisikia simu yangu ikiita.

    β€œMzee mzee, hiyo bwana,” nilisema, mzee akasimama na mimi nikasimama nyuma yake, tukasikia sauti ya mwanaume ikipokea simu yangu:

    β€œHaloo…Juma…Juma gani wewe? Nakuuliza Juma gani maana mimi ndiyo mwenye simu hii, huyo unayemsema simjui na wala hajawahi kumiliki simu hii,” sauti ya kiume ilisema, ukapita ukimya kidogo kisha sauti hiyohiyo ikasema:

    β€œKama unabisha siyo simu yangu ongea na mke wangu huyu hapa.”

    Mara nikasikia:

    β€œHaloo…ni kwa nini mnapenda sana kumfuatafuata mume wangu, mara mzungumzie bangi, mara mtusemee kwa watu.”

    Nilitamani sana kumwambia asiniache katika safari yake maana kwangu kwa muda ule palishaharibika, ningeuawa na watu wasioonekana.

    β€œWewe nisubiri kijana,” mzee aliniambia akiendelea kwenda nje sikukubali.

    β€œMzee humu ndani mimi sikai, nimeshajua sasa.”

    β€œUmejua nini?”

    β€œHuyo Juma anayetajwa hapo nafanya naye kazi na ilikuwa aje na bangi kwa ajili ya hawahawa watu wa humu ndani.”

    Mzee aliniangalia, akaniuliza:

    β€œWewe kijana unaye Mungu?”

    β€œNinaye.”

    β€œHuwa unakwenda kusali?”

    β€œSana.”

    β€œLini umekwenda mara ya mwisho?”

    β€œUngeniambia tatizo ni kusali au?”

    β€œSi hilo tu, ila una matatizo mengi. Hivi hapa tumesimama, nyuma yako nimemuona yule msichana amekuinamia akikung’ong’a kama mara tatu kwa harakaharaka.”

    Nilitimua mbio kuelekea kusikojulikana, nikaenda kufunga breki kwenye mtaa mmoja ambao ukienda kushoto kwangu unakwenda kutokea kwenye barabara ya kwenda Kigogo Mbuyuni.

    Baadhi ya watu walioniona nilivyo walitambua nina tatizo zito kichwani, mzee mmoja aliniuliza kama nakimbizwa nimefumaniwa.

     

    β€œSijafumaniwa mzee, lakini kwa tatizo langu afadhali ningefumaniwa.”

    Huyu mzee alikuwa amebeba kibegi kidogo mgongoni, alivaa suti nyeusi huku akionekana ni mzee mwenye heshima kubwa katika jamii inayomzunguka.

    β€œTatizo nini, hebu nisimulie kidogo tu,” alisema huku akinivutia pembeni. Nilimsimulia kila kitu, alichokuwa akinishangaza sasa, kila hatua ya maelezo yangu alikuwa akiachia tabasamu hata pale nilipoamini kwamba ninachokisema kwa wakati huo asingetabasamu na uso wake ungeonesha kushtuka.

    Nilipomaliza nikanyamaza na kumwangalia kwa woga, nilitaka kuamini ni yule mwanaume aliyepokea simu yangu kule nyumbani amenibadilikia ili nisiweze kumtambua.

    Moyoni nilisema kuwa, kama kweli ni yeye atakapojidhihirishaΒ  tu kwangu nitoke mbio na kwenda kuingia kwenye nyumba ya mtu yeyote mbele yangu.

    β€œTatizo ni hilo dogo tu?” aliniuliza.

    β€œNi hilo tu mzee wangu. Ukiweza kunisaidia nitashukuru sana.”

    β€œNyumba yenyewe iko wapi?”

    β€œKule nyuma nyuma.”

    Nilimwona akiingiza mkono mfukoni na kuchomoa simu nyeusi ndogo, wengi wanaziita za tochi kisha akabonyezabonyeza na kuiweka sikioni. Moyoni nilisema yaleyale.

    β€œSi ajabu anawasiliana na yule mwanamke wa kule nyumbani.”

    Β Nikamsikia akiuliza:

    β€œIsdory, bado mpo hapo?”

    Nadhani huyo jamaa alisema yupoyupo maana nilimsikia huyo mzee akisema: β€œUnaweza kuja na akina Tino hapa kwenye kibanda tulichotuma pesa asubuhi ya leo? Haya njooni.”

    Niligeuzageuza kichwa na kukiona kibanda cha kutuma pesa kwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu. Nikajua amewaita watu waje pale.

    Baada ya dakika kama tatu, wakafika watu kama saba, wanne wanawake, watatu wanaume akiwemo Isdory na Tino.

    β€œHuyu bwana anaitwa,” alianza kusema yule mzee akiniangalia nikajua anataka nijitambulishe jina mimi mwenyewe, nikafanya hivyo. Nilipomaliza, ndipo yule mzee akawaambia wenzake kisa chote cha kwangu, mwanzo hadi mwisho kama nilivyomsimulia awali.

    β€œNdugu, sisi wote walokole, kazi hiyo tunaimudu kwa vile mara nyingi huwa tunatumia jina la Bwana na Mwokozi wetu kufukuza uchafu kama huo, sasa itabidi utupeleke kwenye hiyo nyumba,” alisema yule mzee.

    Nilianza kutembea mimi na wao wakawa wananifuata kwa nyuma. Wale wanawake niliwasikia wakizungumzia mwanamke mmoja aliyeangushwa chini na mapepo akawa anataka kupigana na wale waliokuwa wakimwombea. Moyoni nikasema:

    β€œLeo huko sijui.”

    Tulifika nje ya nyumba, kitendo cha kwanza ambacho si cha kawaida, nilimwona yule kijana muuza maji akitoka ndani. Alivaa kama siku alivyokuja nikamwingiza ndani.”

    Nilishtuka sana, yeye hakushtuka, ila aliponiona akaniambia:

    β€œBro nashukuru sana wamenilipa pesa zangu.”

    Sijui ni nini kilinipata nilijikuta nikisema sawa, sikuongeza neno jingine lolote lile.

    β€œNi humu waheshimiwa,” niliwakaribisha wale watu nikiwa nimeshapishana na yule kijana.

    Waliingia wote ndani, wakasimama katikati ya korido kisha wakawa wananiangalia, yule akaniuliza:

    β€œHivyo vyumba ni vipi?”

    Sikumjibu kwa sauti, nilinyoosha mkono kuelekea kwenye vyumba vyote viwili. Vilioneshwa kufungwa kwa ndani lakini hakukuwa na sauti ya muziki wala maongezi yao.

    β€œBaba katika jina la Yesu,” yule mzee alianza ghafla.

    β€œAmiiiin,” walijibu wote aliofuatana nao, tena walijibu kwa sauti ya juu kisha wakatulia kimya.

    Akaanza kusali akitaja maneno ya kutisha, nilimsikia akisema, choma moto roho mtakatifu, mara Malaika Michael shuka na panga likatalo kuwili.

    Kifupi yule mzee alisema maneno ya ki-Mungu kwa jinsi nilivyoelewa mimi. Ikafika mahali akasema:

    β€œPaaza sauti yako.”

    Ndipo wengine nao wakapokea kwa kila mmoja kuomba kivyake. Wengine walisikika wakisema wanaangusha na kuvunja ngome za ibilisi, wengine wanachoma moto makazi ya shetani, wengine wanamwagia damu ya Yesu pale ndani. Nilianza kuhisi amani iliyoje, niliamini ukombozi umefika tayari kwani sauti tu niliisikia ikipenya hadi kwenye mbavu zangu.

    Waliomba sana, kuna wakati mimi nilihisi kuchoka lakini wao waliendelea tu hadi moyoni nikasema kweli ni watu wa Mungu.

    Ghafla nilianza kuona moshi mweusi ukitoka chini ya milango yote ya wale ndugu, mlango wa sebuleni kama sikikosei na mlango wa chumbani. Moshi ulikuwa mzito kiasi kwamba, kuna wakati nilihisi kupaliwa na kukohoa kwa nguvu lakini wao hawakuonesha dalili ya kusumbuliwa na moshi huo. Nini Kiliendelea? Usikose sehemu ya 09

    Tafadhali Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako Hapo Chini

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoΒ kijiweni.co.tzΒ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiΒ [email protected]Β Β 

    nyumba na majini Nyumba Ya Majini Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni

    29 Comments

    1. Tumpe on June 1, 2024 7:28 pm

      Dooh atatoboa tu

      Reply
    2. Lus twaxie on June 1, 2024 7:36 pm

      Admin tuma nyingne kesho asubuiiiiiii

      Reply
      • Timotheo on June 2, 2024 6:02 pm

        Hii ipo safii admin

        Reply
    3. khamis on June 1, 2024 7:55 pm

      sio powa kutoka kwenye bangi paka maombi

      Reply
    4. Bmt on June 1, 2024 8:01 pm

      Hadithi inatosha sana na pole sana mtu wa mungu

      Reply
    5. Msafiri Mageta on June 1, 2024 8:09 pm

      Adimin kitu ni cha moto sana
      Hongera

      Reply
    6. Godlove4 on June 1, 2024 8:43 pm

      Jina la Yesu ni tiba ya kila jambo

      Reply
    7. Sebeku on June 1, 2024 8:47 pm

      Hao watu wa roho mtakatifu nao wameyatimba yani apo hatoki mtu

      Reply
      • Minnah on June 1, 2024 9:58 pm

        Atatoboa kweli??

        Reply
    8. Sturmius on June 1, 2024 9:18 pm

      Daaah! Kama ni ukweli basi dunia kweli ina mambo! Sema admin unazingua πŸ˜‚ weka hata mbilimbili kila siku aisee..

      Reply
    9. Mabadiliko on June 1, 2024 9:20 pm

      Washampiga sana kizinga sasa wameyatimba🀣🀣🀣🀣🀣🀣 sema ninaogipa hadi kuamka prepo kusoma kisa adith

      Reply
    10. Aspon on June 1, 2024 9:24 pm

      Admin upewe ninileo ili utowe muendelezoπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

      Reply
    11. GODAJA on June 1, 2024 9:30 pm

      Naimani hii ni true storyπŸ₯Ί

      Reply
    12. Ediger on June 1, 2024 9:58 pm

      Watu wameanza kuungua tayari

      Reply
    13. Henderson Didas on June 1, 2024 10:02 pm

      Admin achia nyingine usiku huuπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    14. Faidha on June 1, 2024 10:44 pm

      Yaan naogopa kutoka njeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

      Reply
    15. Fofana on June 1, 2024 11:20 pm

      Admin unatutumia usiku ili na sisi wengine ni waoga, ah admin punguzaa sisi wengine tupo peke yetu, mimi naeka kiporo bana

      Reply
    16. Madam on June 1, 2024 11:48 pm

      Mungu mwema let’s go another episode 😁

      Reply
    17. Dastan on June 2, 2024 12:39 am

      Kumekucha

      Reply
    18. Nagash on June 2, 2024 2:37 am

      Mtunzi nimekuelewa zaidi unapo ikwepa bangi katika kutumiwa big na haijatumika police pia walimpa onyo kali kuhusu bangi unafundisha pia licha tu kua ni story yakuchangamsha ubongoπŸ†

      Reply
    19. Delphina Delphinus on June 2, 2024 5:57 am

      Dah simulizi tamu sana

      Reply
    20. Salumsal on June 2, 2024 9:48 am

      You are incredible things

      Reply
    21. Deroni moresy on June 2, 2024 3:13 pm

      Nataman ingetengenezewa movie natumain ingeuza zaid hap nchini na hata nje ya nchi

      Reply
    22. Ms chunnie on June 2, 2024 5:52 pm

      πŸ˜ͺπŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ’”ni nin lkn mie adii naogopa ahahaha siwaamini wapangaji wenzangu ani baada ya kusoma hii story naota ota🀣🀣… yaaniii nkiamka asubuh nawaangalia wapangaji wenzangu mara mbili mbili

      Reply
    23. Jimmy Gebhard on June 3, 2024 12:15 am

      duuuh! yaan nguvu ya kurudi sijui ningetolea wap???
      n zaidi ya maono ya kidunia

      Reply
    24. Lizzy on June 3, 2024 9:26 am

      πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ m nikajua labda akifika pale atakosa zile nyumba (atakuta nyumba hazipo) 🀣🀣🀣 ila admini ww upo kama LAMATA yaan unatoka nje ya fikra zetu kabisa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… tunaomba uachie mwendelezo mapema sana.

      Reply
    25. Mercy moses on June 3, 2024 10:08 am

      Duh!atatoboa kweli

      Reply
    26. Tina on June 3, 2024 2:37 pm

      πŸ™ Hallelujah

      Reply
    27. Walter on June 4, 2024 10:18 pm

      Hii imekaa vzr Sana πŸ”₯πŸ˜‚

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.