Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (04)
    Hadithi

    Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 28, 2024Updated:May 29, 202416 Comments6 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Nyumba Moja Na Majini
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Nilipoanza kuhisi muda unakwenda na hakuna mtu aliyetoka, nikampa dakika tatu kwamba lazima atakuwa anavaa ndiyo maana anachelewa:

    β€œLabda alikuwa anajisaidia haja kubwa, maana wengine huwa wanavua nguo zote, lakini mimi nipo, siendi kokote,” nilisema moyoni nikiwa bado nimesimama mlangoni kwangu.

    Baada ya muda, nikasikia watu wakiongea chumbani kwao, nikashtuka, nilijikuta nikisema:

    β€œHaa!”

    Haraka sana nilitupa macho mlangoni kuangalia kandambili, nikazikuta pea mbili, nikashangaa: ”

    ENDELEA SEHEMU YA NNEΒ 

     

    β€œIna maana amenipita hapahapa au? Haiwezekani, asingeweza kunipita hata kama ingekuwaje?” niliwaza. Nilitoka kuelekea chooni, nikakuta mlango uko wazi, nikachungulia ndani, hakukuwa na mtu, nikanyoosha mikoni, nikarudi ndani.

    Nilifikia kwenye kochi sebuleni, nikahema kwa nguvu kwani niliamini nimo ndani ya miujiza mikubwa ya ndani ya nyumba ile.

    β€œHivi ni kwa nini dalali alinidanganya hivi?” nilijiuliza mwenyewe nikiamini kwamba, dalali aliyenipangisha nyumba ile alijua mchezo mzima ila alitaka kupata fedha tu ndiyo maana alinipangisha bila kunipa tahadhari.

    Nilitoka sebuleni, nikaenda chumbani, kitandani nikakuta β€˜toilet paper’ ikiwa imekatwa sehemu. Mimi niliicha pembeni ya dirisha, lakini ikaonesha kuna mtu aliichukua na kunyofoa kidogo kisha badala ya kuirudishia palepale, yeye aliiacha kitandani.

    Mbali na β€˜toilet paper’ pia kuna kikopo chenye vijiti vyenye pamba za masikio kilikuwa kwenye stuli jirani na kitanda, lakini kwa muda huo kilikuwa kimeanguka chini halafu vijiti vimebaki kama vitatu tu kwa maana kwamba, aliyeingia kuchukua β€˜toilet paper’ ndiye huyohuyo aliyechota vijiti vya pamba.

    Nilianza kuhisi kuwa sikuwa kwenye nyumba salama, lakini kwa uthibitisho upi? Moyoni nikasema nitajua tu, mimi ndiyo mimi.

    Nilikaa ndani kwangu hadi usiku ulipoingia, nikasema nibadili nguo kwa kuvaa bukta na singilendi halafu nitoke kwenda kula gengeni kwani siku hiyo sikuwa najisikia kupika chochote. Ni mara nyingi nilipenda kula gengeni.

    Nilitoka, nikasimama mlangoni ili nifunge mlango wa chumbani, nilipoangalia chini, upande wa wenzangu nilikuta nje ya mlango wao pana vijiti vya pamba za masikioni vikiwa vimetumika, nikiwa katika mshango, mbele nikaona tishu ikiwa imefutiwa majimaji yenye rangi nyekundu kama damu.

    Nilitembea kwa wasiwasi, nikatoka nje, sikufunga mlango kwa funguo, lakini niliubamiza tu, funguo nilikuwa nazo, nikaenda gengeni kula.

    Pale kwenye genge ambapo si mbali sana na nyumbani, alikuja yule mama aliyeniuliza mimi ni mtu wa wapi, nilimsalimia, lakini kabla hajaitikia alishtuka kuniona.

    β€œUpo kijana wangu?”

    β€œNipo mama, nimetoka kazini nimekuja kupata kidogo.”

    β€œPole sana, uoe sasa.”

    β€œHuo ndiyo mpango wangu mama.”

    β€œEe, uoe halafu mimi nitakupa vyumba viwili pale kwangu, nakuahidi.”

    β€œNashukuru sana mama. Naanza kujipanga.”

    β€œSawa, vipi wenzako lakini?”

    Nilisita kumjibu, nikabaki namwangalia tu, naye alibaini kwamba nimepata mshtuko na swali lake.

    β€œVipi wapangaji wenzako, naamini utakuwa hujaonana nao?”/

    β€œNi kweli mama, tena hebu nakuomba kidogo,” nilisema nikienda pembeni kidogo ili na yeye anifuate tukaongee.

    β€œNiambie,” alianza kusema.

    Nilimuuliza kama kuna anachokijua chochote kile kuhusu wale wapangaji wenzangu. Alianza kwa kusema:

    β€œKusema ule ukweli sina kwa undani, ila napenda kukwambia kwamba, unaishi na watu ambao unahitajika moyo wa ziada ili uweze kuendelea kuishi nao.

    β€œPale mbali na wewe, pameshakaa wapangaji wengine saba, tena wote kama wewe, hawajaoa. Lakini kinachoshangaza ni kwamba, wanaondoka baada ya wiki mbili, mmoja aliondoka baada ya siku tatu tu.”

    β€œKwa hiyo hakuna hata mmoja aliyewahi kukwambia ameona nini kule ndani?”

    β€œHakuna.”

    β€œLo! Mimi mama mambo ninayoyaona yanatisha.”

    β€œKama mambo yapi, nisimulie kidogo.”

    Nilipotaka kuanza kumsimulia huyu mwanamke, ghafla alitokea msichana mmoja, mweupe, mrefu kiasi, amejazia sehemu mbalimbali za mwili, akaguna na kusema:

    β€œKaka Humuli mambo vipi, za siku?”

    Nilipata kigugumizi kikubwa kumjibu mambo poa kwani sikumjua na sikuwa nakumbuka chochote kuhusu yeye, sura yake ilikataa kichwani mwangu.

    β€œWewe ni nani kwani?” nilimuuliza.

    Akaachia tabasamu kwa mbali, uzuri wake ukaongezeka.

    β€œHa! Humuli, hunikumbuki mimi, kweli?”

    β€œSikukumbuki hata kidogo.”

    β€œSasa we binti, kama wewe ndiyo unamkumbuka si umkumbushe mlionana wapi?” yule mwanamke alisema kwa sauti ya mshangao.

    Lakini yule msichana mrembo alimwangalia yule mwanamke kwa macho yaliyojaa hasira…

    β€œMama uhusiki.”

    β€œNajua, lakini unapoteza muda kwa kuzungushazungusha wakati kumbe wewe unamkumbuka, yeye umeshajua hakukumbuki na amekwambia tayari.”

    Nilishangaa kumwona yule msichana akibetua kichwa kama aliyekuwa akiweka vizuri nywele zake, ghafla yule mwanamke niliyekuwa naye akajishika kichwa na kulalamika kinamuuma sana.

    β€œJamani kichwa! Kichwa jamani, daa!”

    β€œVipi mama, imekuwaje kwani?” nilimuuliza.

    β€œKichwa Humuli, kinavuta ghafla! Uwiii.”

    Nilianza kuogopa, nilihisi naangukiwa na msala maana akifa pale na watu waliona nikienda naye pembeni si nitahojiwa mimi?

    β€œKwani mama una kawaida ya kuumwa kichwa?” nilimuuliza nikimsogelea ambapo yeye sasa alikuwa ameinama.

    β€œSina, ndiyo nashangaa hapa.”

    Niliona hakuna dawa nyingine zaidi ya kumpeleka kwake ili nikaungane na familia yake kumpeleka hospitali. Lakini kabla ya kufanya hivyo niliinua macho ili nimwambie yule dada anisaidie na kama anataka kunikumbusha, hayo yangefanyika baadaye.

    Ile naanaza kusema anti huku nikiwa nimeinua macho, nilishangaa kutomwona yule msichana pale.

    β€œKhaa!” nilijikuta nikisema hivyo.

    β€œMama twende nyumbani ili tukupeleke hospitali na watoto wako.”

    β€œHa! Mbona kimeachia,” alisema akionekana kushangaa na kuniangalia, alikuwa amepanua kinywa.

    β€œKweli?”

    β€œEee, niko mzima kabisa.”

    β€œAu?” nilitaka kusema neno lakini zikulimaliza, nikahisi ulimi unakuwa mzito si kwa kushikwa bali kwa matakwa yangu.

    β€œHumuli.”

    β€œNaam.”

    β€œNi kweli yule binti humjui?”

    β€œSimjui mama.”

    β€œKuna mawili hapo, humjui au humkumbuki.”

    β€œVyote mama, simkumbuki na pia simjui.”

    β€œLakini wewe si alikutaja kwa jina?”

    β€œMwenyewe nilishangaa sana.”

    β€œBasi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana,” alisema yule mwanamke huku akiondoka zake kuelekea kwake.

    Nilimtazama, lakini baadaye nilirudi kwenye kibanda cha chipsi.

    β€œMzee nakuona na miss jini,” muuza chipsi mmoja alisema.

    β€œYupi, yule mwanamke?”

    β€œHapana, yule msichana.”

    β€œMi simjui, kwani anaishi wapi? Maana kasema ananijua, ameniita na jina.”

    Β β€œKhaa! Kumbe wewe kama sisi. Huyu dada anaishi mitaa hiihii, lakini hakuna hata mmoja anayejua nyumba anayoishi!

    β€œKuna jamaa mmoja anaitwa Maleke, Maleke aliwahi kumfuatilia kwa nyuma lakini alishindwa kujua aliingia nyumba gani!”

    β€œMh! Au jini?” niliuliza kwa mshtuko mkubwa.

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TanoΒ 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoΒ kijiweni.co.tzΒ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiΒ [email protected]Β Β 

    nyumba na majini Nyumba Ya Majini

    16 Comments

    1. Christed on May 28, 2024 8:14 pm

      Very nice

      Reply
    2. Tyseem on May 28, 2024 8:20 pm

      πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mamb n motooo

      Reply
    3. Jumaa vesso on May 28, 2024 8:27 pm

      uwakika

      Reply
    4. Valence on May 28, 2024 8:37 pm

      Admin weee

      Reply
    5. Yusuf on May 28, 2024 8:59 pm

      Nzuri

      Reply
    6. Pamela Ezra on May 28, 2024 9:11 pm

      Mambo ni moto πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ”₯mwandishi unajuwa

      Reply
    7. Mabadiliko on May 28, 2024 9:14 pm

      Ndo kumekucha Sasa uwhhhh!!!! Zingatia neno MIS JINI

      Reply
    8. Shabani Jumbe on May 28, 2024 9:36 pm

      Ongeza vitisho admin ili iendane na tittle Apo bado haitishi🀣🀣🀣🀣

      Reply
      • Ney gabs on May 29, 2024 6:14 am

        Mmmmh m shaanza kuogopa aaan usiku siigus hii hadith 🀣🀣🀣

        Reply
    9. Nashary m on May 28, 2024 10:15 pm

      Jaman story mzuri Sana

      Reply
    10. Mussa on May 28, 2024 10:39 pm

      Naam Naam patamu sanaaa

      Reply
    11. Vivacious on May 29, 2024 12:12 am

      Hahahaha yaan Utamu siku zote huwa unaishia kati kati daaaπŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ˜‚πŸ˜‚ admin huna baya

      Reply
    12. Sebeku on May 29, 2024 8:18 am

      🌷🌷🌹🌹🌺πŸ₯€ admin chukua maua yako hakika unatukosha haswa

      Reply
    13. Muuh on May 29, 2024 6:18 pm

      Mungu wangu

      Reply
    14. Samson on May 30, 2024 10:54 am

      Amaizing

      Reply
    15. Official DG on May 30, 2024 1:19 pm

      Admini nakubali kazi zako lakini napenda kukwambia hili igizo lisha igizwa na kurushwa sinema zetu… Ila kazi iendelee

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.