Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Aheri Ya Inonga Mgonjwa Kuliko Mabeki Wengine Simba Wazima
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Aheri Ya Inonga Mgonjwa Kuliko Mabeki Wengine Simba Wazima

    Nazareth UpeteBy Nazareth UpeteApril 23, 2024Updated:April 23, 20247 Comments2 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Henok Inonga Simba Sc
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Mpira wa miguu ni mchezo wa hisia sana kwani ni moyo ndio huzungumza kuliko hata mdomo lakini kubwa tunalopaswa kufahamu ni kuwa palipo na hisia kubwa kuna mstari pia wa kifo na uhai na ndio hapo hapo anaingia Henock Inonga na mashabiki wa Simba

    Niseme tu kuwa soka ni kama mahusiano ya mapenzi ambayo huchipua popote na wakati mwingine mtu anaweza kupoteza hamu na kukitaka kitu kwa sekunde kadhaa tu! Ni mchezo wa kinafiki flan hivi.

    Sio mbali sana kwani kuna barua iliandikwa hapa Kijiweni kuhusu Henock Inonga na nitanukuu kifupi “Inonga ni mchezaji mzuri mno… Masikhara yake au kujiamini sana akiwa na mpira vinaweza kuja kuharibu uhusiano wake na Simba SC…”

    Bahati mbaya naona mada imegeuka ghafla na naona watu wanamshutumu kuwa alijivunja mechi dhidi ya Yanga SC lakini nikiri tu kuwa sifahamu sana hilo labda watu wanajua zaidi.

    SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga

    Wakati wa kupasha misuli moto kwa mazoezi madogomadogo siku ya dabi ya Kariakoo ni wazi kuwa alikua akionesha mashaka kwamba hawezi kumaliza ile mechi kwani alikua anaonekana kwamba hayupo ngangari zaidi kwa mchezo dhidi ya Yanga kutokana na kutokua fit

    Baada ya mechi Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola akasema Inonga aliumia siku kadhaa mazoezini na walimchezesha wakiwa wanajua hilo Tafsiri yake!? “Aheri ya Inonga mgonjwa kuliko mabeki wengine wa Simba wazima”. Jamaa akiwa kwenye ubora wake ni daraja kubwa barani Afrika Tangu arudi AFCON anasemwa kwenye namna ngumu na ya kufikirisha huku wengine wanasema kabisa bora aondoke.

    Ndio njia ya mpira wa miguu kwani wale wale walionisemea maneno mabaya na makali niliposema ana masikhara kwenye maeneo ya msingi leo wanataka aondoke na hapa ndio unaona kwamba Mpira una kijiunafiki flan ivv!

    Mapenzi yakifika ukomo ndio utaanza kusikia harufu ya kibeberu kwa Bwana wako ama kusikia shombo la Samaki ozo kwa Manzi yako Mara chache Mapenzi yakaisha vyema… Muda mwingi huisha Kwa taabu

    Naendelea kuamini kuwa ni Mapenzi tu ya mashabiki na Inonga yamefika mwanzo wa mwisho wao lakini Who will survive!? Henock… Ni miongoni mwa mabeki Bora wa kati waliopita nchini! Kwenye hili atatoboa!? Ni muda tu utasema kweli!

    inonga kuondoka simba? inonga simba sc simba sc tanzania

    7 Comments

    1. Niornky on April 23, 2024 2:43 pm

      Apoo na kubaliana na wew kabisa lakin kwa upande wangu Inonga nibeki moja safii sana ata akienda katika timu yoyote kubwa basii ata kuwa katika kikosi cha kwanza kuliko mchezaji yoyote pale Simba ni beki la viwango sana.

      Reply
    2. John mussa on April 23, 2024 2:52 pm

      Ndio inonga ni beki Bora sana pale simba

      Reply
    3. [email protected] on April 23, 2024 3:11 pm

      Inonga ni mchezaji mzuri na mkubwa lakini Kuna mambo mengine anayafanya Hadi mdogo wake Salim mwenyewe anabaki anashangaa … Mpira WA siku hizi hautaki ucheze sana na jukwaa especially eneo anavocheza yeye ndo mana Ibra bacca alivowachukua chama n’a saidoo hakuwainua mashabiki Bali alifanya kuutoa mpira katika eneo lile sipati picha angekuwa Huyu mkojani…

      Reply
    4. ๐—ง๐—ฎ๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ถ ๐—”๐—ฏ๐—ฏ๐—ฎ๐˜€ on April 23, 2024 3:13 pm

      Unamaanisha kuwa ๐—ถ๐—ป๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ฎ ndie beki bora na bila yeye ๐˜€๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ sii chochote?…lahasha!!! ๐—ง๐—ฒ๐—ฎ๐—บ kiujumla ni mbovu kuanzia uongozi mpaka wachezaji wake.

      ๐—ง๐—ฎ๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ถ ๐—”๐—ฏ๐—ฎ๐—ฎ๐—ฎ๐˜€

      Reply
    5. Paul Emmanuel on April 23, 2024 3:16 pm

      Kiukweli henock ni beki bora sana ila aheri asiondoke ila aletewe mshindani mwingine kwenye nafasi yake kwasababu saivi akiondoka hapatakuwa na replacement yauhakika out of kazi Ko Bora
      Abaki aletewe mpinzani

      Reply
    6. Fredi0 on April 23, 2024 3:56 pm

      Inonga pale man utd anamuweka Maguire nje

      Reply
    7. Eve on April 24, 2024 11:00 am

      Hakika Inonga chuma , ila Wekundu wamezingua aisee wanatuumiza mashabiki Kuna watu wanaingizwa uwanjani kitimiza wajib tuu ila ubora ni zero percent, Kuna yule alikuwa anachangamsha team na walimuweka sub Kila match na akiingia anafanya maajabu ila wamemtoa #Moses Phiri๐Ÿ˜ญ

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneย  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.