Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika
    Africa | CAF

    Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika

    Living ShayoBy Living ShayoFebruary 5, 20243 Comments3 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ni zaidi ya miongo mitatu sasa tangu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kuanzishwa na kushuhudia  mataifa mbalimbali yakipokezana taji hili hasa yale ambayo yana wastani mzuri wa wanasoka wanaosukuma kabumbu  nje ya bara la Afrika.

    Mwaka 2023, Taifa la Ivory Coast limebahatika kuandaa AFCON ya 34 huku Mataifa yenye Idadi kubwa ya wachezaji wanaokipiga kwenye Ligi za ndani ya bara hili wakionesha Mapinduzi makubwa na  kutingisha vigogo kadhaa huku toleo hili la 34 la AFCON limekuwa tofauti wengi wa waafrika waliamini mataifa ambayo yana wachezaji wengi wanaocheza nje ya bara ili wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ukilinganisha na mataifa ambayo vikosi vyao vimeundwa zaidi na wazawa wanaocheza Ligi za nyumbani kwao pamoja na ndani ya bara la Afrika.

    Imekuwa tofauti sana kwani sehemu kubwa ya wachezaji waliyofanya vizuri wanacheza Ligi za ndani ya bara la Afrika kama Henock Inonga wa DR Congo, Percy Tau wa Afrika Kusini, Djigui Diara kutokea Mali, Aliou Dieng wa Mali, Ali Sangare wa Ivory coast na zaidi ni kuwa Afrika ya Kusini imeheshimisha Ligi za ndani ya bara la Afrika ikiwa klabu pekee yenye wachezaji wengi wanaokipiga Ligi za ndani ya bara hili.

    Wanaturudisha nyuma na kutupa kumbukumbu ya Spain iliyokuwa na wachezaji wengi wanaokipiga ndani ya Spain huku robo tatu ya kikosi kikiwa ni cha FC Barcelona. Mpaka wanafika hatua hii ya nusu fainali robo tatu ya kikosi chao kinaundwa na wachezaji wanaocheza klabu ya Mamelodi Sundowns ya nyumbani Afrika kusini.

    Shujaa wa hatua ya nusu fainali Ronwen Williams, mabeki Aubrey Modiba, Mothobi Mvala, Grant Kekana, Khuliso Mudau, viungo Teboho Mokoena, Themba Zwane pamoja na Thapelo Morena na hawa wachezaji huwa ndiyo waliocheza sana kwenye kikosi hicho cha Bafana Bafana.

    Lakini kikubwa zaidi ni kuwa kikosi chote cha Afrika Kusini “Bafana Bafana” kinaundwa na wachezaji kutoka vilabu saba vya Afrika kusini na kimoja nje ya taifa ilo huku wachezaji wawili (2) tu kutokea nje ya bara la Afrika ambao ni kiungo Mihlali Mayambela kutokea Aris Limassol ya Cyprus pamoja na kiungo Sphephelo Sithole kutokea Tondela ya Ureno.

    Vilabu ambavyo vimefanikiwa kutoa wachezaji ndani ya kikosi hicho kutokea PSL ni Pamoja na Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Amazulu, Cape town City, Polokwane city, Stellenbosch FC pamoja na Sekhukhune United. Kumbuka kuwa Afrika Kusini ndiyo taifa ambalo limefuzu hatua ya nusu fainali na wachezaji kutokea Bara la Afrika tofauti na Nigeria yenye wachezaji wengi kutokea nje, Ivory Coast na DR Congo pia. Huu ni wakati sasa kujiamini kuwa bara la Afrika tunaweza na vipaji tunavyo lakini pia ni fundisho kuwa siyo lazima kuwekeza kwa wachezaji wanaocheza nje ya bara la Afrika bali ni njia nzuri za kimpira kuanzia uwekezaji, imani, uvumilivu na kujitoa kwa wasimamizi wa mpira ndani ya nchi husika.

    SOMA ZAIDI: Inonga Kuondoka SIMBA Baada ya AFCON? 

    afcon AFCON 2023

    3 Comments

    1. Pingback: Ratiba Kamili Nusu Fainali AFCON - Kijiweni

    2. Pingback: Ukiizungumzia Nusu Fainali AFCON Huwezi Yaacha Majina Haya - Kijiweni

    3. Pingback: Wachezaji Watano Muhimu Wa Kuwapa Ubingwa Ivory Coast - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.