Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Huwezi Amini AFCON Imepita Na Vichwa Vya Makocha Hawa
    Africa | CAF

    Huwezi Amini AFCON Imepita Na Vichwa Vya Makocha Hawa

    Living ShayoBy Living ShayoJanuary 27, 20241 Comment3 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kocha mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche ambaye AFCON imemla kichwa
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Wakati hii leo ni rasmi kuwa hatua ya 16 bora inaanza lakini michuano ya AFCON msimu huu imekuwa ya tofauti sana na wengi ambavyo walitarajia itakuwa, na hii ni kutokana na baadhi ya mataifa makubwa kufanya vibaya kwa kushindwa kupata matokeo kwa mataifa ambayo yalionekana madogo kwao na hayana uwezo wa kuwafunga.

    Hiyo imesababisha makocha kutoka mataifa hayo kufukuzwa na baadhi yao kujiuzulu wenyewe kutokana na mataifa yao kufanya vibaya na mengine yakishindwa kufuzu hatua ya 16 bora, makocha hao ni ;-

    1.DJAMEL BELMADI (ALGERIA)

    Kocha huyu ana umri wa miaka 47, alikuwa anafundisha kikosi cha timu ya taifa ya Algeria ambapo alianza kuinoa timu ya taifa ya Algeria mwaka 2018 na mwaka 2019 alifanikiwa kutwaa ubingwa wa AFCON nchini Misri.

    AFCON ya msimu huu imekuwa mbaya kwake kwani katika michezo 3 ya makundi aliyosimamia kikosi hicho amefanikiwa kukusanya alama mbili tu akipata sare michezo 2 na kufungwa mmoja.

    Djamel Belmadi alifungashiwa virago muda mfupi tu baada ya mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Mauritania ulipomalizika na kupoteza kwa goli 1-0 na kufanya kushika mkia kwenye kundi lao.

    2.CHRIS HUGHTON (GHANA)

    Kocha huyu mwenye miaka 65 akiwa na uraia wa England alianza kuinoa timu ya taifa ya Ghana mwaka 2023 akichukua mikoba ya Otto Addo. Ghana ilikuwa kundi B pamoja na Misri, Msumbiji na Cape Verde, hata hivyo kikosi chake kilikusanya alama 2 tu katika michezo 3 ya makundi na kupelekea kufukuzwa na Shirikisho la Soka Ghana na moja ya sababu ni kushindwa kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

    3.JEAN LOUIS GASSET (IVORY COAST)

    Mzaliwa wa Ufaransa na Mchezaji wa zamani akiwa na miaka 70, alianza kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ivory Coast mwaka 2022. Licha ya timu hiyo kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya AFCON kama “Best Looser” ila Shirikisho la Mpira nchi humo chini ya Raisi Yacine Idriss Diallo ilimfungashia virago Kocha huyo licha ya kikosi hicho kuwa wakitandaza kandanda safi na hiyo ni kutokana na wakiamini walipaswa kufuzu vizuri zaidi ya hapo.

    4.TOM SAINTFIET (GAMBIA)

    Kocha huyu mwenye miaka 50 akiwa na uraia wa Ubelgiji alianza kuinoa Timu ya taifa ya Gambia mwaka 2018. Tamati ya kuinoa timu ya taifa ilo ilifikia Januari 23,2024 baada ya kufungwa goli 3-2 na kumaliza hatua ya makundi wakiwa hawajakusanya alama hata moja na kupelekea kujiuzulu kwa Kocha huyo muda mchache tu baada ya mchezo dhidi ya Cameroon kutamatika. Huyu ndiyo Kocha pekee aliyejiuzuru mwenyewe baada ya timu anayoifundisha kufanya vibaya.

    5.JALEL KADRI (TUNISIA)

    Ana miaka 52 akiwa na uraia wa Tunisia alianza kuifundisha timu ya taifa ya Tunisia mwaka 2022.Kushindwa kufuzu hatua ya mtoano ya michuano ya AFCON licha ya Taifa ilo kupewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa ikawa sababu tosha ya kujiuzulu kwa Kocha huyo.

    Jalel Kadri ameiongoza michezo 3 ya makundi akifanikiwa kukusanya alama 2 sawa na Sare 2 huku akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Namibia na kupelekea kushika mkia kwenye kundi E lililokuwa na timu za taifa za Mali, Afrika Kusini na Namibia.

    6.ADEL AMROUCHE (TANZANIA)

    Ni raia wa Algeria akiwa na miaka 55 tu na alianza kuinoa timu ya taifa ya Tanzania mwaka 2023.Huyu  yake ipo tofauti kwani yeye alisimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania baada ya kukumbwa na rungu la kufungiwa michezo 8 na Shirikisho la Soka Afrika baada ya kutoa Lugha zilizokuwa zinashiria utovu wa nidhamu kwa timu ya taifa ya Morocco.

    Huyu bado hajafukuzwa ila alisimamishwa na haijulikani kama ataendelea kuinoa timu ya taifa ilo au atafungashiwa virago.

    SOMA ZAIDI: Nilitegemea Haya AFCON Hatua Ya Makundi

    makocha afcon

    1 Comment

    1. Pingback: Namibia Imetuonesha Umuhimu Wa Kumuamini Kocha Mzawa - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.