Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Saido, Chama wakatishwa Likizo, Waitwa Fasta Klabuni
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Saido, Chama wakatishwa Likizo, Waitwa Fasta Klabuni

    David MohamedBy David MohamedJuly 3, 2023No Comments3 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama na Shomary Kapombe walikuwa wakila bata makwao kipindi hiki cha mapumziko, lakini ghafla wakapigiwa simu na mabosi wao na kutakiwa kukatisha likizo hizo na fasta watue jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa michuano.

    Sio Chama na Saido tu, bali hata wachezaji wengine 21 wa kikosi cha sasa cha timu hiyo wakiwamo kipa Aishi Manula anayejiuguza kwao mjini Morogoro naye ametakiwa kufika Dar kama ilivyo kwa Kibu Denis, Shomary Kapombe, Ismael Sawadogo, Habib Kyombo na John Bocco.

    Nyota hao wa Simba wameitwa na mabosi hao kwa ajili ya vipimo vya afya watakavyochukuliwa kuanzia kesho kwa kundi la wachezaji wazawa kabla ya kuhamia kwa wageni, kisha kufuata nyota wale waliosajiliwa na kikosi hicho akiwamo Leandre Willy Onana Essomba aliyetoka Rayon Sports.

    Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, mabosi wa Simba wameamua kuwaita wachezaji wote ili kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya safari ya nje ya nchi zikitajwa Afrika Kusini au Uturuki itakapowekwa kambi ya maandalizi ya msimu mpya kulingana na maelekezo ya Roberto Oliveira.

    Kundi la kwanza la wazawa litakalopimwa kuanzia Jumatatu, linahusisha wachezaji 12 waliopo kikosi cha sasa akiwamo nahodha John Bocco, Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Kibu Denis, Ally Salim, Ahmed Feruzi Teru, Israel Mwenda, Mzamiru Yasin, Jimmyson Mwanuke, Nassor Kapama, Habib Kyombo na Mohamed Mussa.

    Kundi la pili litakalojumuisha wachezaji 10 wageni na kipa Aishi Manula aliyetoka kufanyiwa upasuaji hivi karibuni Afrika Kusini, litafanyiwa vipimo Jumanne likiwa na Ismael Sawadogo, Moses Phiri, Joash Onyango, Sadio Kanoute, Jean Baleke, Saido, Chama, Henock Inonga, Peter Banda na Pape Ousmane Sakho.

    “Haya ni maandalizi ya kuanza safari ya kwenda kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya, kocha kataka wote wafanyiwe vipimo mapema kisha zianze taratibu za safari ya kwenda kuweka kambi ya msimu mpya, kisha naye atajumuika wiki chache zijazo sambamba na nyota wapya walisajiliwa na watakaosajiliwa,” alisema mmoja wa vigogo wa klabu hiyo aliyeomba kuhifadhiwa jina.

    Kigogo huyo alisema wito huo unajumuisha wachezaji wote bila kujali kana kuna waliopo kwenye hesabu za kupewa ‘Thank You’, kwa vile hadi sasa hakuna maamuzi mengine yaliyofanyika baada ya kutemwa kwa nyota wanane Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Beno Kalolanya na Gadiel Michael.

    Wageni waliopigwa chini hadi sasa ni Wanigeria Nelson Okwa na Victor Akpan, Mghana Augustine Okrah na Mohamed Ouattara kutoka Burkina Faso, huku Ismael Sawadogo, Joash Onyango na Peter Banda wakitajwa wapo kwenye mazungumzo kutokana na kuwa na mikataba inayowabana.

    Onyango inaelezwa ameomba kuondoka Msimbazi, huku Peter Banda na Sawadogo wakikomaa wakitaka kuvunjiwa mikataba kama hawapo kwenye mipango ya kocha Robertinho na sio kupelekwa kwa mkopo katika klabu nyingine. Kwa wazawa Kennedy Juma anatajwa kuwa nyota wa tisa kupewa ‘Thank You’ baada ya kugoma kuongeza mkataba kwa kilichoelezwa yupo mbioni kutua Singida BS ndio maana jina lake halikuwekwa kwenye orodha ya nyota hao waliokatiziwa likizo zao ili waje Dar.

    clatous chama kapombe kibu denis saido ntibazonkiza Simba simba sc
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.