Tuko katika kipindi ambacho ligi mbalimbali duniani zinaelekea ukingoni huku zipo ligi ambazo mabingwa tayari wamekwishajulikana lakini zipo ligi ambazo mabingwa bado hawajajulikana na ndio kipindi ambacho mchezaji au wachezaji hujituma kuhakikisha kuwa wanaipa mafanikio klabu ambayo wanaichezea.
Hivi sasa tupo ukingoni kabisa mwa ligi lakini pia ndio kipindi ambacho timu zinafikiria namna ya kuboresha vikosi vyao kulekea msimu mpya unaofata katika kuhakikisha kuwa wanatekeleza malengo yao ambayo unaweza kukuta katika msimu husika wameshindwa kuyatekeleza au wameyatekeleza lakini wanataka kuboresha zaidi.
Hiki ndio kipindi ambacho pia kumekua na tetesi nyingi sana kuhusiana na mchezaji au wachezaji ambao wanakua wamemaliza mikataba yao au inakaribia kuisha lakini pia ndio kipindi ambacho kumekua na tetesi kuhusiana na klabu ambazo zimekua zikiwahitaji wachezaji flani huku kukiwa na taarifa mchezaji huyu anaenda timu gani.
Swali langu ni dogo sana kwako mwana KIJIWENI kutokana na tetesi ambazo umekua ukizisikia lakini pia kuhusu mchezaji ambae yupo katika timu ambayo wewe unaishabikia unadhani kwenye timu yako mchezaji gani akiondoka kwako fresh tu na wala haina shida na akiondoka katika timu yako akaenda kwenye timu ambayo huikubali yaani huishabikii bado utaendelea kumsapoti mchezaji huyo?
Lakini pia ukipata nafasi ya kuongea na uongozi wa timu yako utatamani nani asajiliwe?
Unapenda SIMULIZI? Gusa Hapa Sasa Kusoma KOTI JEUSI
