NECTA yatangaza matokeo ya Kidato cha Nne 2025, kiwango cha ufaulu chafikia asilimia 94.98

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) wa mwaka 2025, mtihani ambao ulianza rasmi Novemba 17, 2025.

Matokeo hayo yametangazwa siku ya Jumamosi, Januari 31, 2026, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohammed.

👉 Angalia matokeo ya Kidato cha Nne hapa

Jumla ya watahiniwa 569,883 kutoka shule 5,864 zilizosajiliwa walifanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2025, huku watahiniwa binafsi 25,927 wakisajiliwa katika vituo 813.

Katika taarifa iliyotolewa Novemba 16, 2025, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohammed, alisema idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa asilimia 7.67 ikilinganishwa na mwaka 2024.

Kati ya watahiniwa 569,914 wa shule waliosajiliwa, 266,024 walikuwa wavulana sawa na asilimia 47, huku 303,859 wakiwa wasichana, sawa na asilimia 53.

Mahudhurio ya mtihani yalifikia asilimia 97.5, sawa na watahiniwa 555,606.

👉 Angalia matokeo ya Kidato cha Nne hapa

Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha ufaulu kwa ujumla kimeongezeka kwa asilimia 2.61, kufikia asilimia 94.98, ambapo watahiniwa 526,620 walipata Daraja la Kwanza hadi la Nne (Divisheni I–IV).

Idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya juu (Divisheni I–III) pia imeongezeka hadi 255,404, sawa na asilimia 46.1 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

SOMA RIWAYA ZA KIJIWENI Kwa Kugusa Hapa 

2 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version