Wengi wamekua wakiamini kuwa ni kama imekuwa kama dharau kwa mzawa kocha Juma Mgunda kila timu inapopoteana (mwendelezo mbovu) na makocha wa kigeni kutimuliwa au kuondoka katika timu ya Simba huwa inamkumbuka Juma Mgunda na kumpa timu tena.
Nani asiyejua uwezo wa Juma Mgunda katika ligi hii?Hakuna ambaye hata kidogo anaweza kuwa na hofu juu ya uwezo wa wake na wengi wa wapenzi wa soka Tanzania wanaamini kuwa ni muda rasmi wa Simba kumuamini na siyo wakufanya kibarua cha saidia fundi ila anastahili kupewa timu kama kocha mkuu, na kitu kikubwa ni yeye kama kocha kuendelea kudumaza uwezo wake kwa kuendelea kung’ang’ania Simba SC ingawa kwa wakati mwingine unaweza kusema pia ni maokoto.
Ndiyo, Mgunda siyo kocha wa kwenda kufundisha wanawake au kwenda kufundisha vikundi vya vijana tena vijana wenyewe wanatengenezwa kisiasa tu lakini ukija kwenye uhalisia ni uongo mtupu.
Mgunda atapewa heshima yake endapo ataondoka simba sc na kwenda kufundisha timu nyingine za ligi kuu kama ambavyo aliifanya klabu ya Coastal mpaka kufika fainali ya kombe la FA, Namungo nk, maana anaweza kuwa kocha mkuu kwenye timu yoyote ukitoa Simba na Yanga ambazo zinaamini katika makocha wa kigeni zaidi.
Maoni yangu: Binafsi ninaheshimu sana uwezo wa kocha huyu ila kitendo cha kupewa timu kila makocha wanapoondoka siliungi mkono na kumuona Mgunda hana msimamo bali anafurahi sana kuwa saidia fundi.
SOMA ZAIDI: Fredy Ni Mchezaji Mzuri Akitumiwa Vizuri Ataisaidia SIMBA
