Mimi naomba nitofautiane kidogo na wadau wengi wa Kijiweni hasahasa mashabiki wa timu hizi kubwa yaani Yanga pamoja  mashabiki wa Simba ambao  wanadai Fredy Koublan ni garasa ingawa anafunga vizuri tu pale ambapo akipata nafasi japokua huwa kuna makosa baadhi ambayo huwa yanajitokeza pale ambapo anakosa magoli. Huyu mchezaji namfananisha na The Great Khali (kwa walioangalia mieleka miaka ya 2005 watakua wanamjua vilivyo)

Kwanza ana mwili mkubwa, ni mrefu, ameshiba pia ana nguvu ni kama the great khali ambaye ushindi wake WWE huupata kwa faida ya umbo lake na mwili wake, mbinu na ufundi sifuri, akikutana na beki ambaye ana mwili mdogo huwa ndio utaona balaa lake zaidi.

Fredy huwa anasumbua sana mabeki akiwa na mpira ni ngumu kumpokonya maana ana nguvu kama kifaru ila hana skills nzuri za kufunga, hupenya kirahisi ndani ya 18 na ni vigumu kumpiga .mtama au kumsukuma akaanguka, ili kuweza kumshinda inabidi akabwe na watu wanne azingirwe pande zote. Beki kitasa BACCA alimshindwa akafunga, magoli mengi anayofunga ni ya kuwashinda nguvu mabeki.

Ushauri wangu huyu mwamba achezeshwe namba 10 kwa sababu hiyo namba inahitaji mtu mwenye misuri na anayeweza kupenya kirahisi ukuta wa beki zote za kati na pembeni, Atafutwe namba tisa mwingine mwepesi mwenye mbio na Simba itapata matokeo ya haraka

SOMA ZAIDI: Tukiyafanya Haya Kiwango Cha Mpira Tanzania Kitapanda

Leave A Reply

Exit mobile version