Kwako Mo Dewji
Natumai barua hii inakufikia wewe na familia yako katika afya njema na ustawi wa kiroho na kimwili. Napenda kutumia fursa hii kuelezea mawazo yangu na kufikisha ombi muhimu kuhusu uwekezaji ndani ya klabu ya Simba.
Hakuna ambaye hafahamu kuwa Simba ni mojawapo ya klabu kubwa na ya kihistoria katika soka la Tanzania. Klabu hii imekuwa ikileta furaha na shauku kwa mamilioni ya mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hata hivyo, ili klabu iendelee kustawi na kufikia viwango vipya vya mafanikio, inahitaji uwekezaji mkubwa zaidi katika miundombinu, vifaa vya michezo, na maendeleo ya vijana.
Kupitia uzoefu wako na ujuzi wako katika uwekezaji, ningependa kuwasilisha ombi la kuzingatia uwekezaji ndani ya klabu ya Simba na wala sipingani na jinsi ambavyo umekua na mchango mkubwa katika mafanikio y klabu hii,lakini tambua kuwa uwekezaji mkubwa zaidi utasaidia kuboresha miundombinu imara na kuweza kuanzisha programu sahihi za maendeleo ya vijana, na kuimarisha kikosi cha Simba ili iweze kushindana kikamilifu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
Kwa ninayoyaona niwazi niseme kuwa mashabiki wamekosa imani kubwa kwa Try Again na Mangungu kwani wanaamini kuwa hawaujui mpira na fitina zake na ndio maana sasa hivi Simba imekuwa katika kipindi hiki cha kupata matokeo kwa shida. Na inaonekana kama vile watu wanaojua mpira Simba na wanaoweza fitina za mpira wakina Magori na Kaduguda japo bado wapo Simba lakini ni kama vile wamekaa pembeni wanatazama jahazi linavyozama. Hata Simba kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi mwaka huu ikiwa chini ya uongozi wa Try Again na Mangungu kwa kweli itakuwa ni bahati sana.
Mwisho kwa nini Try Again na Mangungu wasiwe waungwana tu wakajiuzulu ili waingie watu wengine wenye uwezo wa kuivusha Simba itoke hapo ilipo. Wanang’ang’ania nini kuongoza Simba wakati toka waingie kwenye uongozi Simba imepoteza makombe yote chini yao na hakuna dalili ya kupata hata moja msimu huu.
SOMA ZAIDI: Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda
