Kilichofanywa na mchezaji Fiston Mayele ichukuliwe kama funzo kwa sajili zingine. Nafiriki viongozi wa Yanga SC hawakuwahi kujifunza juu ya baadhi ya nyota ambao hua wanawasajili kisha kuwavua nguo na baadae wanawarejesha tena klabuni.
Wapo ambao wameonyesha kufurahishwa sana katika hili tena wengine wameenda mbali kukenua mimi niwapa pole sana kwasababu mambo mabaya kama hayo hua hayadumu. Si tuliona mfano mdogo kwa Feisal Salum kisha baadae ikaibukia kwa mshambuliaji Prince Dube, kwani imechukua muda gani basi.
Upendo kwa Mayele ulikuwa mkubwa tena alipewa kila kitu, siyo kutetemesha watu kila alipokwenda alikuwa kama mfalme. Hakuna mchezaji aliyeongoza kwa kupewa zaidi kumzidi yeye. Ng’ombe alipewa, U- Chief aliupata pesa pia sasa sijui ni kipi kilimpata mchezaji huyu.
Naamini tukianza kuelezana mabaya hapa hakuna Klabu itakayosimama lakini wachezaji wanaamua kuyafukia mambo kwenye kifua. Kazini hua haya yanajitokeza sana sema ni vile watu wanayatiliza vifua kama mipira kisha maisha yanasonga.
Tuziandike takwimu na tuzidadavue kwa ukubwa lakini lazima tukubali ndugu yetu ameteleza na ameonyesha ameshindwa kuyavumilia mambo, amekubali kukiachia kifua chake kibaki wazi, kolomelo la KIUME limemponyoka hata hivyo Tanzania hatuna baya haya yote sisi tunafukia tu kisha maisha yanaendelea kama ilivyo tamaduni yetu, kwetu sisi wageni ni wetu.
Karibu tena FISTON KALALA MAYELE katika ardhi iliyobarikiwa kila kitu, amani, starehe, upendo hata na ukarimu pia, tunakupenda na wala hatukuchukii, ulichoshindwa ni kutenganisha utani wa mpira na maisha halisi.
SOMA ZAIDI: Naamini Kuwa Mchawi wa Simba ni Wanasimba Wenyewe
