Viongozi wa Simba wanajiroga wenyewe na kujitega kwenye mtego mbaya kwa mashabiki wao kwani ukitazama tu mtiririko wa namna ambavyo kumekua na mabadiliko ya makocha ndani ya klabu hiyo inaonesha kuwa kuna shida mahali ambayo inawafanya mashabiki kutokua na imani na viongozi wao.

Kama ulikua hufahamu ni kuwa Simba wameendelea kuachana na makocha wao kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na katika miaka hiyo 3 imekua katika mtiririko huu hapa :

 

Novemba 2021 – Mei 2022

Pablo Franco

 

Juni 2022 – Septemba 2022

Zoran Mac

 

Septemba 2022 – Januari 2023

Juma Mgunda

 

Januari 2023 – Novemba 2023

Roberto ‘Robertinho’ Olivieira

 

Novemba 2023 – Aprili 2024

Abdelhak Benchikha

 

Hii inashiria kwamba kuna shida ndani ya uongozi wa Simba na shida kubwa kuna presha ya kutaka kuendelea kupata mafanikio ambayo waliyapata kwa kipindi cha misimu minne mfululizo lakini hadi sasa kumekuwa na kuyumba kwa mafanikio hayo ambayo yanapelekea hata makocha kufukuzwa au makocha kuvunja mkataba na klabu hiyo

Lakini pia ukitazama ishu ya kuondoka kwa Benchikha si ishu ya mojakwa moja ya matatizo ya kifamilia bali inaonyesha ni makubwa wanayaoyataka Simba lakini hayaendani na uwekezaji waliouweka kwa msimu huu,ikiwemo wachezaji ambao walikuwepo Simba kwa sasa ilikuwa inamuonyesha kocha anawakati mgumu zaidi kufikia kile Simba sc wanachokitaka na ukizingatia hali ya muendelezo wa matokeo yaliyopo licha ya kubeba kombe la Muungano.

Uongozi wa Simba unapaswa kufahamu kuwa mpira kuna kipindi unaweza ukapitia kwenye wakati mgumu na kwenda nje kabisa ya malengo yao lakini nafasi ipo kwao kujipanga vizuri na kila mmoja atimize majukumu yake bila kuingilia majukumu ya mtu mwingine anaye husika katika usajili wamuache afanye usajili ulio sahihi kwa tafsiri ya kocha ndiye awe na jukumu hilo kwa kushirikiana na skauti aliyekuwepo klabuni hapo .

Pia watafute kocha mkuu mapema kabla msimu haujaisha ili apate nafasi ya kuchunguza timu na kuanza kusuka timu ambayo italeta ushindani mkubwa zaidi kwenye mashindano yote ikiwemo ile ya kimataifa.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa:

1.Je wanaohusika kufukuza na kuajiri makocha simba kwenye misimu yote hiyo si ndiyo hao hao viongozi wapo je wao hawana matatizo? Mbona hawawajibiki.

2.Kama kubadili makocha kuna tija mbona kuleta mataji ya ubingwa hatuyaaoni.?

SOMA ZAIDI: Waraka Mzito Wa Hamisi Kigwangalla Kuhusu “Kuinunua Simba”

Leave A Reply

Exit mobile version