Tajiri, kijana wako niliendelea kusubiri ile Suuu lakini mpaka sasa bado hujasema lolote, Tajiri mimi bado nasubiri. Najua moyo wako ulivyo na mapenzi mema na Simba SC basi tupe hii Boss. Mohamed Dewji nakiri wazi uliamua kwa dhati kutuonyesha tukiamua inawezekana, uliifanya Simba SC kuwa tishio Afrika na kucheza Robo Fainali nne Ligi ya Mabingwa huku moja ikiwa ni kombe la Shirikisho na juzi kati hapo imecheza tena ya tano lakini hadithi ni ileile tu. Tajiri Mohamed Dewji, kilio cha wanasimba ni kuwavusha kwenda Nusu fainali, rudi tena kazini wape furaha ya namna hiyo, njoo tena utoe darasa la kwenda hatua hiyo pengine tutafika. Ukweli wa wazi wewe ndiye mtu uliyethubutu kwa dhati kuwaonyesha matajiri wengine inawezekana wakiamua. Hapa naandika kama mdau wa soka lakini mtu ambaye nakubali sana kazi zako, njoo tena na tena tuelekeze tunafuzu vipi hiyo Nusu mbona ni kama manyanyaso yamezidi. Itazame Al Ahly na Mamelodi Sundowns kwanini waonekane ni kikwazo, KWANINI ionekane haiwezekani, njoo tena Tajiri tunakusubiri. Simba SC imeweka alama Afrika hilo halina ubishi, hakuna atakaye toka na kulikataa hili sidhani hayupo huyo mtu. Mo Dewji imeiweka ramani ya mpira wetu katika Chapa ya Moto naamini ipo siku tutafika tu. Naiweka chini KALAMU yangu nasubiri kuona au kusikia tena SUUUU imebeba nini Tajiri. Unatamani Tajiri MO DEWJI Afanye kitu gani ili kuhakikisha Simba inarudi ile ambayo tumeizoea? Acha comment yako hapa chini

Leave A Reply

Exit mobile version