Kibu Denis Prosper ndio ajenda iliyopo mezani kwa sasa na Tanzania nzima ipo mezani kujadili mada hii! Kwanza sipo hapa kuzungumza kuhusu Takwimu za Mchezaji wala kuchagua upande wowote kuhusu hili bali nasimama hapa kwenye uhalisia

Sidhani kila mmoja kama anajiuliza maswali haya ninayojiuliza Mimi!  Moja, Je ni kweli Thamani inayotajwa inafaa kusimama kwa Mchezaji husika? Je, hiyo pesa ambayo anahitaji ni sahihi Simba kuitoa kwa sasa? Tatu, Simba hawawezi kupata mchezaji mzuri kwa pesa hiyo? Nne, Kwanini Simba matukio ya hivi yananirudia sana? Simba wanahitaji kutoka wapi na kwenda wapi?

Baada ya kumaliza kujibu maswali hayo nadhani umeanza kupata picha taratibu, binafsi sina upande wowote ila ukweli ni kwamba nyakati kama hizi Menejimenti nyingi za wachezaji ndio sehemu zao na wanajua namna ya kucheza nazo ukikaa vibaya utashindwa kwenda njia sahihi kwa wakati huo kutokana na msukumo uliopo nje

Kinachofanywa ni mchezaji kupandishwa Thamani kwa Mchezaji ambapo mara nyingi Timu Pinzani, Waandishi wa habari na Vyombo vya habari na vingine hutumiwa kwa kiasi kikubwa sana kusukuma Thamani ya kitu husika kwa wakati huo hivyo usipokuwa makini utaacha njia yako na utatembea kwenye njia yao bila kujua

Labda nitoe vitu vichache tu ambavyo vinafanya Thamani ya mchezaji kuwa kubwa ambapo vichache ni Umri wa mchezaji husika, kiwango chake kwa wakati huo na Thamani ya mkataba wake kwa sasa! Chukua hivyo vitu vichache kisha vitumie kwenye mada iliyopo mezani kuhusu Kibu Denis ndani ya Simba SC halafu chukua hapo juu vile vitu ambavyo nisema vinatumiwa kupandisha Thamani ya mchezaji

Last! Kama unahitaji kupiga hatua kubwa kutoka ulipo basi kuna muda ni lazima kukubali kufanya maamuzi magumu ambayo yataendana na mipango yako kwa wakati husika, THAMANI DHIDI YA MABADILIKO 🇹🇿

Let’s Go!!.

SOMA ZAIDI: Simba SC Na Roho Ngumu Kwa Mtibwa Sugar Ligi Kuu

Leave A Reply

Exit mobile version