Baadhi ya tetesi zinadai kuwa huenda kiungo wa Zambia na mchezaji wa Simba Clatous Chota Chama anaweza kujiunga na klabu ya Yanga akitokea Simba. Klabu ya Simba haijafanya juhudi zozote za kumuongezea mkataba mchezaji huyo na tetesi nyingi zikidai tayari klabu ya Yanga imeshaweka donge nono mezani kwajili ya usajili wa kiungo huyo

Kama Chama atajiunga na miamba hiyo yaani mabigwa wa kombe la NBC Premier League (Yanga) ataongeza upana wa kikosi na kufanya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Miguel Gamondi kuwa na wachezaji watatu wa kariba moja na wenye uwezo wa kucheza namba 10 uwanjani kwa ufasaha.

Swali ni je kama Yanga watamnasa Chama ipi ni hatima ya Aziz ki na Pacome kama watalazimika kubaki muundo wa uchezaji wa Yanga utakuwaje nani atapata nafasi ya kucheza nafasi ya namba 10 yani kiungo mshambuliaji nyuma ya striker namba 9 namba ambayo wachezaji wote watatu wanakuwa huru sana wakiicheza.

Kwanza pichani hapo juu ni muonekano wa eneo la kati hadi mbele litakavokuwa kama chama atafanikiwa kujiunga na yanga sasa tudadavue msitari wa Chama, Aziz Ki na Pacome utachezaje

Kwanza nikuhakikishie kuwa wachezaji wote hao watatu wanaweza kucheza katika nafasi ya namba 10 ndani ya mechi moja kwa lugha ya kisoka inaitwa (Triple ten) au (3 10’s) tujue ili kucheza namba kumi watatu unahitaji nini.

Kitu cha muhimu ni kuwa unahitaji namba kumi wawili wenye uwezo wa kucheza maeneo ya pembeni na kufanya mikimbio kwenye eneo la kati kwajili ya kutengeneza idadi ya namba kumi 3 nikukumbushe Chama na Saido walicheza kama namba 10 wawili Simba msimu jana Saido akisimama kama namba kumi asilia na Chama akitokea eneo la namba 7 na mikimbio kuelekea namba 10

Pia nikukumbushe Pacome na Aziz Ki wamewahi kucheza kama namba kumi wawili Pacome akitokea eneo la namba saba au kumi na moja hivyo wachezaji wote hao watatu wanauwezo wa kufanya ivoo kucheza pembeni kisha wakakimbilia kati kutengeneza namba 10 3 tazama

Hivi ndivyo Yanga watacheza kama wakiamua kutumia namba kumi watatu (Lomalisa na Yaoyao watatumika kama mawinga muda wa kushambulia muda ambao Pacome na Max wataingia katikati ) Swali kwa kocha Je kikosi kitakuwa na uwiano mzuri muda wa kushambuliwa yaani wakiwa hawana mpira hii nitaelezea kwenye andiko lijalo itakuwa mada pana ya Yanga akiwa na mpira na bila ya mpira muundo wao wa kiuchezaji

Swali ni Je Nani anafaa kuanza nafasi ya namba kumi kwa maoni yako Chama, Pacome au Aziz Ki?  

SOMA ZAIDI:  Je Simba Wana Mradi Mpya Au Wanataka Kurudisha Wa Zamani?

Leave A Reply

Exit mobile version